DHAMBI YA DHARAU


 Mithali 14:21

Kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa dharau ni dhambi kama dhambi zingine.

Kuna aina kuu mbili za dharau

1. Dharau ya moyoni yaani mtu anamdharau mwingine moyoni mwake (2 Samweli 6:16)

2. Dharau ya waziwazi

(Mathayo 26:67)

DALILI ZA MTU MWENYE DHARAU

1. Kebehi au dhihaka (Luka 16:14)

2. Kujihesabia haki (kujiona bora kuliko wengine) (Luka 18:9-14) kwa mfano kuna watu huwa wanajifanya wao ndio wanaongea na Mungu mtu mwingine akisema jambo aliloambiwa na Mungu atapingwa ataonekana ametunga mawazo yake.

3. Kuwasema watu vibaya au kumteta au kumsengenya mtu (Hesabu 12:1-2)

 Miriam na Haruni waliponzwa na dharau hatimaye Miriamu akapigwa kwa ukoma.

4. Kukosa shukrani (Luka 17:12-19)

 Kukosa shukrani ni sawa na kudharau kilichotendwa kwako.

5. Migomo (Esta 1:10-22) Vashti aliitwa na Mfalme akakataa kuja (aligoma)

6. Mzaha (2 Wafalme 2:23-24)

7. Kufyonya au kufyolea (Mathayo 5:22)(Zaburi 22:7)

BAADHI YA WATU WALIOPONZWA NA DHARAU

1. MIKALI (MKE WA DAUDI)

Alimdharau mumewe na alikufa hana mtoto (2 Samweli 6:16-23)

2. TAJIRI ALIYEMLISHA LAZARO MAKOMBO (Luka 16:19-31)

Kilichomfanya huyo tajiri akajikuta kuzimu ni dharau, alimdharau Lazaro.

Ukitaka kujua huyu mtu alikuwa na dharau, alitambua duniani kuna watumishi lakini aliwadharau akataka atumwe mtumishi kutoka kwa wafu ili akahubirie ndugu zake.

Ibrahimu alikataa akasema huko duniani wapo watumishi wa Mungu, ndugu wa tajiri wasipowasikiliza hao watumishi walioko hai duniani basi watakuja Kuzimu.

3. MIRIAM (Hesabu 12:1-10)

Miriamu na Haruni Walimteta Musa kuhusu mwanamke aliyemuoa, hatimaye Miriamu alipigwa kwa ukoma.

4. MALKIA ESTA 

(Esta 1:10-22)

Aliitwa na Mfalme akakataa kuja, aliondolewa kwenye nafasi ya umalkia.

5. GOLIATHI (1 Samweli 17:42-54)

Alimdharau daudi akadhani daudi hawezi kumfanya chochote lakini alijidanganya kabisa. 

Chapisha Maoni

0 Maoni