Heshimu watu hata yule ambaye unadhani hana cha kukusaidia na yule ambaye unadhani hana manufaa kwenye maisha yako.
Unajua ni kwa nini uheshimu watu?
1. Anaweza akawa hana cha kukusaidia ila anaweza kukukumbusha umesahau kufunga zipu ya suruali yako au umeangusha tiketi yako.
2. Maisha yanabadilika, wa nyuma anaweza kuja mbele na wa mbele akarudi nyuma.
3. Hakuna anayejizika akifa, kila mtu huzikwa na wengine.
4. Anaweza akawa na taarifa nyeti unayoitafuta kwa muda mrefu au taarifa ya kukufanikishia mpango wako.
5. Anaweza akawa anapajua unakoenda, ukipotea njia anaweza kukuelekeza njia ya kupita.
0 Maoni