Mwanamume, usije kusahau hili neno aliloambiwa Mzee wetu Adamu.
"kwa kuwa umemsikiliza mkeo................" Mwanzo 3:17-19
Hilo neno lina mafunzo mengi ikiwemo:-
1. Usimpe nafasi maishani mwako mwanamke yeyote ambaye anamsikiliza shetani.
2. Usimwamini mwanamke ambaye hamuamini Mungu - kitendo cha mwanamke kula lile tunda ni ishara inayodhihirisha kumwamini Shetani.
-Mwanamke yeyote ambaye anaishi kinyume na neno la Mungu ni hatari kwa mwanamume yeyote.
3. Mwanamke yeyote asiyetambua nafasi yako kama mwanamume ni hatari kwako mwanamume, kitendo cha mwanamke kula lile tunda kilikuwa ni kitendo cha ukaidi na kutokumuamini mumewe aliyepewa maagizo ya kutokula yale matunda ya ule mti na akamfundisha mkewe.
4. Mwanamke yeyote ambaye hamtii Mungu hawezi kukutii wewe, mwanamke huyo ni hatari kwako mwanamume, kama anajifanya kukutii lakini hamtii Mungu basi ujue huo ni utii wa maigizo.
5. Matatizo ya mwanamume (Adamu) yalisababishwa na mwanamke ambaye yuko kinyume na Mungu, hivyo basi mwanamke yeyote ambaye yuko kinyume na neno la Mungu ni hatari kwako na atakusababishia mabalaa.
6. Hawa alikuwa mwanamke mwema kabisa lakini alipokubali kumtii shetani aligeuka kuwa mwanamke mbaya kwa mumewe, hivyo basi ni vema ufahamu kuwa unaweza kuoa mke mwema lakini akijikuta amemtii shetani anaweza kuwa mwanamke mbaya sana kuliko Yezebeli mke wa Mfalme Ahabu wa kule mashariki ya kati.
7. Mungu alimwambia Adamu "kwa kuwa umemsikiliza mkeo" maana yake ni kwamba mwanamke aliyemuasi Mungu hatakiwi kusikilizwa, ukimsikiliza tarajia kupatwa na mabalaa.
KAMA IMEFIKA HATUA MKEO AMEVURUGWA UFANYEJE?
1. Busara inaniongoza tusizungumzie sebuleni UTAKUJA CHUMBANI (INBOX) KAMA UTAONA VEMA.
2. Tafuta watumishi wa Mungu wakusaidie.
0 Maoni