FASIHI SIMULIZI KAMA NYENZO YA UFUNDISHAJI WA NENO LA MUNGU

 Yesu alikuwa mhubiri na mwalimu wa neno la Mungu, nyenzo mojawapo aliyotumia katika kufundisha ni FASIHI SIMULIZI.

Alikuwa akifikisha ujumbe wake kupitia simulizi mbalimbali alizokua akisimulia watu.

Kwa mfano

●Yesu alisimulia kuhusu mkopeshaji alivyowasamehe watu aliokuwa anawadai (Luka 7:40-50)

●Alisimulia kuhusu Lazaro na tajiri (Luka 16:19-31)

●Alisimulia kuhusu mtu aliyekuwa akisafiri akavamiwa na majambazi (Luka 10:30-37)

NB: Nyenzo mojawapo unayopaswa kuizingatia wakati unafundisha neno la Mungu ni FASIHI SIMULIZI.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni