✍Faraja Gasto
(Zaburi 78:3-7)
Jambo mojawapo ambalo Mungu aliwaagiza wana wa Israeli ni KUWAAMBIA WATOTO WAO MAMBO ALIYOYATENDA (FASIHI SIMULIZI).
Hiyo ilihusisha historia jinsi walivyokuwa watumwa kule nchini Misri na jinsi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani na matendo ya ajabu aliyoyatenda.
Hili ni jambo ambalo walilishika, wakawa wakiwasimulia watoto wao mambo ambayo Mungu alitenda.
(Waamuzi 6:13)
Kijana aitwaye Gideoni alikiri kuwa baba zao waliwahadithia matendo ya ajabu ambayo Mungu aliyatenda kule Misri na aliyowatendea waisraeli.
Kizazi cha wakina Gideoni walifahamu matendo yale ya ajabu ya Mungu kwa kuwa walisimuliwa na baba zao.
FUNZO
Tukitaka kutengeneza kizazi kinachomjua Mungu ni muhimu kutumia fasihi simulizi kama mbinu mojawapo ya kufikisha ujumbe kwa kizazi, tuwasimulie watoto na vijana mambo ambayo Mungu aliyatenda au aliyowatendea watu mbalimbali.
●Ukiwa na watoto wako au vijana wako wasimulie mambo ambayo Mungu alikutendea.
●Wasimulie mambo ambayo Mungu aliwatendea watu wengine ambao habari zao zimeandikwa kwenye Biblia.
●Wasimulie mambo ambayo Mungu aliwatendea watu unaowafahamu.
NB: Jambo hilo litajenga kitu ndani yao hata kama hautaona matokeo yake wakati huo, WEWE SIMULIA TU.
0 Maoni