UNAPOSHIRIKI MEZA YA BWANA


Kama unashiriki meza ya Bwana na bado umejaa chuki, uchungu na visasi hiyo ni ishara mojawapo inayoonyesha haujui unachofanya.

Hivi unajua pale msalabani Yesu alikuwa anaondoa uadui kati ya watu na Mungu kupitia mwili na damu yake? (Waefeso 2:16)

Hivi unajua damu na mwili wa Yesu una nguvu ya kuondoa uadui?

Kama mwili na damu ya Yesu viliondoa uadui kati ya watu na Mungu, unadhani mwili na damu ya Yesu vinashindwa kuondoa uadui kati ya mtu na mtu? kati ya jamii na jamii? kati ya ndugu na ndugu?

Chapisha Maoni

0 Maoni