MWILI NA DAMU YA YESU KAMA CHANZO KIMOJAWAPO CHA NGUVU ZA KUWAPATANISHA WATU NA MUNGU


(Waefeso 2:16)

Yesu alitoa mwili na damu yake ili kutupatanisha na Mungu.

Yesu ametupa huduma ya upatanisho ili tuwapatanishe watu na Mungu (2 Wakorintho 5:18-20)

Tunapokula mwili wa Yesu na kunywa damu yake (meza ya Bwana) kwa imani tunapata faida mbalimbali ikiwemo "kupata nguvu za kuwapatanisha watu na Mungu" 

NB: Yesu alitupatanisha na Mungu kwa mwili na damu yake kule msalabani lakini sisi tunawapatanisha watu na Mungu kupitia injili, wanapoamini injili wanapatana na Mungu.

Hivyo basi ni vema ufahamu kuwa mwili na damu ya Yesu ni chanzo kimojawapo cha nguvu za kuwapatanisha watu na Mungu kwa kuwa damu na mwili wa Yesu vilitolewa kwa ajili ya upatanisho (kuwapatanisha watu na Mungu).

Unapoula mwili wa Yesu na kunywa damu yake kwa imani utafahamu kuwa upendo wa Mungu ndio ulipelekea kutolewa kwa mwili na damu ya Yesu, ukishafahamu hilo UTAKUWA NA NGUVU YA KUWASHUHUDIA WENGINE HABARI ZA YESU KRISTO ALIYEWAPENDA NA KUJITOA KWA AJILI YAO  ILI KUWAPATANISHA NA MUNGU.

Chapisha Maoni

0 Maoni