KUJITENGA NA WATU WABAYA


(2 Wakorintho 6:14-18)

UTANGULIZI
Biblia inatuambia kuwa hapa duniani kuna watu wabaya (Habakuki 1:4)(2 Timotheo 3:13)(Ufunuo 2:2)(Yeremia 15:21)

Watu wabaya ni watu;-
â–ªWanaowaza mabaya (Mwanzo 6:5)
â–ªWanaozungumza mabaya (1 Wakorintho 15:33)
â–ªWenye ushauri mbaya (Ezekieli 11:2)
â–ªWenye mwenendo mbaya (Waefeso 4:17)

NAMNA YA KUJITENGA NA WATU WABAYA
â–ªUsiige mienendo yao au usifuatishe mienendo yao (3 Yohana 1:11)(Warumi 12:1)(Ezra 9:1)

â–ªUsifanye urafiki na watu wabaya (2 Wakorintho 6:14-18)(1 Wafalme 3:1)(2  Mambo ya Nyakati 18:1)

â–ªUsiende kwenye mabaraza yao (Zaburi 1:1)

BAADHI YA FAIDA ZA KUJITENGA NA WATU WABAYA
â–ªNi kwa ajili ya usalama wako.
(Mwanzo 19:12-25)
Lutu alijitenga na watu wa Sodoma, baada ya hapo miji ya Sodoma na Gomora ikateketezwa, asingekubali kujitenga nao angeangamia kule Sodoma.

â–ªMungu atakufurahia na kukutumia (2 Timotheo 2:21)

â–ªKwa ajili ya kutunza maadili yako, ya jamii nakadhalika.
(2 Wakorintho 15:33) Biblia inasema mazungumzo mabaya yanaharibu tabia njema.

Watu wabaya huzungumza mambo mabaya unapojitenga na watu wabaya unaepuka kuharibika kwa mwenendo wako.

Chapisha Maoni

0 Maoni