UTANGULIZI
Agano ni kiapo cha kutenda au kutotenda jambo fulani (Isaya 54:9)(Mwanzo 9:11)(Kutoka 32:11-14)
Kwa hiyo mtu anapoapa huwa anafanya agano fulani.
Kwa mfano Rais huwa anaapa kulinda katiba, lile ni agano.
Watu huwa wanaapa mahakamani nakadhalika, kiapo ni agano.
IKO HIVI: Watu wengi wamekuwa hawanufaiki na maagano yaliyowekwa na Mungu kutokana na sababu mbalimbali.
Mungu aliyeziumba mbingu na nchi ni Mungu ashikaye maagano
(2 Mambo ya nyakati 6:14)(Danieli 9:4).
Kilichosababisha wana wa Israeli wakatoka nchini Misri kwenye utumwa ni agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu, Isaka na Yakobo (Kutoka 2:24).
Mungu alipolikumbuka agano lake ndipo akamtuma Musa kwenda kuwatoa nchini Misri.
Wana wa Israeli walinufaika na agano lile na wakatoka nchini Misri.
AGANO LA AMANI (Isaya 54:10-17)(Ezekieli 34:25-31, Ezekieli 37:26-27)
Agano la amani ni agano ambalo Mungu alifanya na wana wa Israeli, agano lilihusu mambo mbalimbali ikiwemo; kuwalinda, kuwabariki, kuwazidisha, kuwaokoa na maadui zao, hawatakufa kwa njaa, uwepo wake utakuwa nao nakadhalika.
NAMNA YA KUNUFAIKA NA AGANO LA AMANI
1. Lifahamu agano lenyewe kama nilivyoeleza kwa ufupi hapo juu.
2. Fahamu kuwa wana wa Israeli sio tu wale wayahudi bali hata sisi tuliomwamini Yesu Kristo ni wana wa Israeli kwa imani (Wagalatia 3:29)
3. Mkumbushe Mungu agano lake.
--Musa alimkumbusha Mungu agano lake na Ibrahimu, Isaka na Yakobo (Kutoka 32:11-14) Mungu alipokumbuka akaacha kuwaangamiza wana wa Israeli.
Na wewe unaweza kumkumbusha Mungu agano lake la amani, Mungu hukumbuka agano (Kutoka 2:24).
Barikiwa kwa hayo machache.
0 Maoni