KILIMO CHA BUSTANI

 

(Mwanzo 2:8,15)

Mungu ndiye mwanzo wa kilimo, aina ya kilimo ya mwanzo kabisa ni kilimo cha bustani.

Mungu alianzisha kilimo cha bustani kwa manufaa ya mtu aliyemuumba.

Mungu alimuweka mtu (Adamu) ili alime na kuitunza bustani, humo ndimo palikuwa makazi yake na ofisi yake (kazini kwake) ambapo alikuwa anajipatia chakula.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Sokoine  cha kilimo kilichopo Tanzania, wanasema "kilimo cha bustani kinahusika na uzalishaji wa mazao ya aina ya
mboga, matunda, viungo na mimea ya mapambo".

Biblia inatujulisha kuwa Mungu alipanda bustani iliyokuwa na matunda nakadhalika kwa ajili ya mtu, pia wapo watu ambao wamewahi kuwa na Bustani kwenye makazi kwa ajili ya kupamba makazi, kulima matunda nakadhalika.

Kwa mujibu wa Biblia kilimo cha Bustani kinahitaji mambo ya msingi yafuatayo-
●Eneo (Mwanzo 2:8)

●Unachopanda au mbegu (Mwanzo 2:9)

●Maji kwa ajili ya umwagiliaji (Mwanzo 2:10)

●Nguvu kazi kwa ajili ya usimamizi wa bustani (Mwanzo 2:15)

NB: Kama una ardhi au una eneo unaweza kujihusisha na kilimo cha bustani kwa ajili ya kupata mboga, matunda, mahali pa kupumzika nakadhalika.

Yapo mambo mengi ya kujifunza kuhusu kilimo cha aina mbalimbali kwenye Biblia ikiwemo kilimo cha bustani, nakuhimiza kusoma Biblia ili ujifunze ikiwa unapenda kilimo.

Niishie hapo 👆👆👆

Chapisha Maoni

0 Maoni