JINSI YA KUFAHAMU IKIWA MUNGU AMEJIBU MAOMBI YAKO


 ✍Faraja Gasto

Lengo la somo hili ni kukufahamisha ishara ambazo zinaonyesha Mungu amejibu maombi.

Biblia imeweka wazi kuna uwezekano mtu akajibiwa maombi lakini asijue kama amejibiwa maombi yake.

(DANIELI 9:23)

Danieli ajibiwa maombi yake lakini hakujua kama amejibiwa akaendelea kuomba.

NB: Si vibaya kuendelea kuomba ila ni vema ufahamu ishara zinazoonyesha Mungu amejibu maombi ili iwe rahisi kuepuka kuendelea kuomba jambo ambalo tayari Mungu amejibu.

Zipo ishara nyingi ambazo  zinazoonyesha  Mungu amejibu maombi ila nitafundisha jambo moja ambalo ni AMANI YA KRISTO.

USHUHUDA

Wakati fulani nilikuwa ninahitaji fedha kiasi fulani nikachukua hatua ya kumuomba Mungu.

Wakati naendelea kuomba niliona amani imetawala moyoni mwangu, huzuni niliyokuwa nayo ikatoweka nikasikia amani, nikajua tayari Mungu amejibu nikaacha kuombea jambo lile.

Baada ya siku chache Mungu alifanya njia nikapata fedha nilizokuwa nazitaka.

IKO HIVI: Mungu alitumia amani ya Kristo kunijulisha kuwa tayari amejibu ninachoomba.

Amani ya Kristo ni ishara mojawapo inayoonyesha Mungu amejibu maombi yako, wakati unaomba au baada ya maombi ukiona amani ya Kristo imetawala moyoni mwako fahamu kuwa Mungu ameshajibu, achana na hicho unachoombea, ombea mambo mengine.

Barikiwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni