✍Faraja Gasto
DADA, BINTI, MWANAMKE wakati unasubiri kuolewa ni vema ujifunze mambo mbalimbali yatakayokusaidia kwenye ndoa.
Baadhi ya mambo unayopaswa kujifunza ni:-
●Jifunze ujuzi wa mawasiliano katika ndoa Ili ujue namna ya kuwasiliana na mumeo.
Jambo mojawapo linaloharibu ndoa nyingi ni mawasiliano mabovu kati ya mke na mume, mawasiliano mazuri yanalinda ndoa.
Sifa mojawapo ya mke mwema ni ujuzi wa mawasiliano (Mithali 31:26)
●Jifunze kupika.
--Kuna tofauti ya kujipikilisha na kupika, kujipikilisha ni kupika ilimradi au kupika ovyoovyo, jifunze mapishi ili ujue kupika kwa kuwa utakuwa na wajibu wa kumpikia mumeo na wageni watakaowatembelea.
Wajibu wa kumpikia mumeo ni wa kwako sio wa msaidizi wa kazi.
Mke unapaswa kujua vyakula anavyopenda mumeo na uvipike kwa ustadi (Mwanzo 27:9,14)
●Jifunze kuishi na watu.
--Kumbuka mumeo naye ni mtu ana hulka zake na tabia zake.
--Wanadamu tuna hulka na tabia tofautitofauti ni vema ujifunze kuishi na watu.
--Kuna wakati unaweza kujikuta unapaswa kuishi na shemeji zako, mawifi, mama mke au baba mkwe nakadhalika kwa muda fulani na wana hulka na tabia tofautitofauti kuna wengine hulka na tabia zao utazifurahia na wengine tabia na hulka zao zitakukera lakini utatakiwa kuishi nao.
(1 Samweli 25:1-3)
Abigaili alikuwa mke wa Nabali, Nabali alikuwa na tabia zisizo nzuri lakini Abigaili alijua namna ya kuishi na mumewe.
●Jifunze kuhusu usaidizi kwa kuwa unatarajiwa kuwa msaidizi.
--Kwa mfano Roho Mtakatifu anaitwa msaidizi (Yohana 15:26)
Roho Mtakatifu hutusaidia mambo mengi ikiwemo udhaifu wetu (Warumi 8:26) kumsaidia mtu udhaifu wake ni kuhakikisha udhaifu wa mtu hauwi sababu ya mambo mbalimbali kukwama, hauwi sababu ya mtu kupata matatizo.
--Roho Mtakatifu kama msaidizi hutukumbusha mambo mbalimbali.
Hivyo basi wewe kama mke mtarajiwa,
--Huwezi kumsaidia mtu udhaifu wake kama haujui udhaifu wake hivyo basi wewe kama mke mtarajiwa ni vema uanze kuyafahamu madhaifu ya mume wako mtarajiwa ili ujue namna ya kumsaidia.
--Utapaswa kuwa mtu wa kumkumbusha mumeo mambo mbalimbali.
●Jifunze kuhusu kiumbe anayeitwa mwanamume.
(Mwanzo 2:7)
--Ni vema ujifunze kuhusu mwanamume ili ujue nafasi Mungu aliyompa na mamlaka aliyopewa nakadhalika.
●Jifunze sana neno la Mungu (Wakolosai 3:16)
●Jifunze sheria ya ndoa kwenye Biblia.
--Sheria ya ndoa ina vipengele vingi baadhi ya vipengele ni hivi vifuatavyo;-
1. Utapaswa kumtii mume wako (Waefeso 5:22-24)
2. Unapaswa kuwa na mwenendo mzuri ili uwe mfano wa kuigwa (1 Petro 3:1-6)
3. Mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe (1 Wakorintho 7:4)
Leo niishie hapo 👆👆
0 Maoni