✍Faraja Gasto
UTANGULIZI
Yapo mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye dunia wakati huu mengine ni mabaya kabisa.
Yapo mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye nchi yako wakati huu mengine ni mabaya kabisa.
Yapo mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye jamii wakati huu mengine ni mabaya kabisa.
--》Mambo hayo mabaya yanapaswa kutengenezewa mikakati ya maombi ili yasilete madhara mbalimbali.
(DANIELI 2:1-10)
Mfalme Nebukadneza alitoa amri wenye hekima wote wa Babeli wauawe, miongoni mwa wenye hekima wa Babeli walikuwemo akina Danieli na wenzake.
Danieli alipopata taarifa ya mpango wa kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli aliwajulisha wenzake WAKATENGENEZA MKAKATI WA MAOMBI (Danieli 2:17-18)
Mkakati ule wa maombi uliwaepusha wenye hekima wa Babeli wasiuawe pia ulisababisha Danieli na wenzake wakapandishwa vyeo kazini (Danieli 2:46-49)
(ESTA 4:1-17)
Baada ya Hamani kuhitilafiana na Mordekai aliandaa mpango wa kuwaangamiza wayahudi wote.
Mordekai alipofahamu mpango huo (Esta 4:1) alianza mawasiliano na Esta ili kuona namna ya kukabiliana na mpango huo hatimaye WALIKUBALIANA KUTENGENEZA MKAKATI WA MAOMBI (Esta 4:15-17)
Mkakati ule wa maombi uliwaepusha wayahudi wasiangamizwe, mkakati ule ulisababisha Mordekai akapata heshima kubwa (Esta 6:6-12) pia mkakati ule wa maombi ulisababisha Malkia Esta akapewa nyumba ya adui yao (Esta 8:1)
KUFAHAMU YANAYOENDELEA
Tunapofahamu mambo yanayoendelea kwenye nchi, jamii, kazini nakadhalika ndipo tunaweza kutengeneza mikakati ya maombi ili tuombe kwa ufanisi.
Ili tufahamu yanayoendelea lazima
●Tuwe wafuatiliaji wa taarifa za habari.
●Tuwe wafuatiliaji wa matangazo.
●Tuwe wasomaji wa machapisho mbalimbali (Esta 4:7-8)
●Tutafute kujua yanayoendelea kwa kuuliza (Esta 4:5-8)
●Tuwe wafuatiliaji wa mipango mbalimbali.
UMUHIMU WA KUFAHAMU YANAYOENDELEA
●Inatusaidia kutengeneza mikakati ya maombi.
●Inatusaidia kuepuka maangamizo na uharibifu mbalimbali, kwa mfano kama Danieli na wenzake wasingefahamu yanayoendelea kule Babeli wasingeombea jambo lile lenye madhara ni hakika wangeuawa kwa kuwa wao pia walikuwa miongoni mwa wenye hekima wa Babeli.
HITIMISHO
Jambo mojawapo linaloweza kutusaidia kuomba kwa ufanisi ni kufahamu yanayoendelea kwenye nchi, jamii, kazini nakadhalika.
Hivyo basi baada ya kufahamu yanayoendelea ni vema kutengeneza mikakati ya maombi kwa ajili ya usalama wako, watu wengine, jamii, nchi nakadhalika.
0 Maoni