✍Faraja Gasto
(Yakobo 4:8)
UTANGULIZI
Mtume Yakobo aliandika waraka huu kwa watu ambao ilifika hatua walimpa shetani nafasi na jambo hilo likawapelekea kuanza kupigana, kuoneana wivu, kuuana nakadhalika (Yakobo 4:1-7)
Mambo hayo yaliwafanya wakajitenga mbali na Mungu, jambo mojawapo alilowaambia ni "Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili" (Yakobo 4:8)
Ukweli ni kwamba Mungu hayuko mbali, Mungu yuko karibu (Yeremia 23:23)(Isaya 55:6) lakini watu ndio hujiweka mbali na Mungu (Mathayo 15:8)
NAMNA YA KUMKARIBIA MUNGU (KUWA KARIBU NA MUNGU)
Haya ni mambo baadhi yatakayokusaidia kuwa karibu na Mungu.
1. Mwamini Bwana Yesu - Okoka.
(Waefeso 2:13) Biblia inasema mtu akimwamini Yesu Kristo anakuwa karibu na Mungu.
2. Epuka dhambi.
"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili" (Yakobo 4:8)
Hata kama umeokoka lakini kama unaendelea kuishi dhambini ujue unajitenga na Mungu.
3. Kusikiliza na kujifunza neno la Mungu.
(Luka 10:38-42)
Watu wanaosikiliza na kujifunza neno la Mungu hujiweka karibu na Mungu.
4. Maombi.
(Isaya 55:6)
Mungu tunaweza kumkaribia kwa njia ya maombi.
5. Ibada.
Mungu alituumba ili tumwabudu yeye, kuabudu kunapaswa kuwa mtindo wetu wa maisha, tunapaswa kumuabudu Mungu kila siku.
Baadhi ya mbinu za kumuabudu Mungu ni;-
●Kuutoa mwili wako kuwa dhabihu kwa Mungu (Warumi 12:1)
●Kumsifu Mungu.
(Zaburi 119:164) Mfalme Daudi alikuwa anamsifu Mungu mara saba kila siku.
Kusifu ni sehemu ya ibada.
BAADHI YA FAIDA ZA KUWA KARIBU NA MUNGU
1. Mungu ataongea na wewe na kukushirikisha mambo yake.
(Mwanzo 18:22-23)
Ibrahimu alishirikishwa na Mungu mpango wake wa kuangamiza miji ya Sodoma na Gomora kwa kuwa alikuwa karibu na Mungu.
2. Utamjua Mungu.
Wanaomjua Mungu ni watu walio karibu naye.
(Yohana 8:55)
Yesu alisema anamjua Mungu Baba kwa kuwa alitoka kwake (Yohana 7:29)
Viwango vyetu vya kumjua Mungu vinategemea na viwango vya ukaribu tulionao na Mungu.
0 Maoni