KUONWA: WARAKA KWA WANAWAKE WANAOTAKA KUOLEWA


DADA, BINTI, MWANAMKE si kila aliye mzuri anaolewa.

Kuolewa ni matokeo ya mambo mbalimbali ikiwemo KUONWA.

KUOLEWA NI SUALA LA KUONWA

"Mke mwema, ni nani awezaye KUMWONA? Maana kima chake chapita kima cha marijani" Mithali 31:10.

Kuna wengine mkionwa na wanaume, ndani ya wanaume kunaumbika picha wanaona kahaba si mke, wanaona mpiga mizinga si mke, wanaona wewe sio wa hadhi yake, wanaona haufai kuwa mkewe, wanaona tapeli si mke nakadhalika.

Kuonwa tofauti ni matokeo ya uchawi, tabia zako chafu, muonekano wako na namna watu wanavyokuzungumzia.

NB: Wengine ili muolewe mnahitaji maombezi na kufunguliwa kutoka kwenye vifungo, wengine mnapaswa kuboresha tabia zenu na wengine mnapaswa kubadili mionekano hususani kwenye eneo la mavazi.

Chapisha Maoni

0 Maoni