KIJANA NA MWELEKEO WA MAISHA


 ✍Faraja Gasto

(ZABURI 119:9)

Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.

Andiko hilo lina swali na lina jibu la swali husika. 

Andiko hilo linatupa picha ya maisha ya vijana, vijana wana maswali mengi wanayojiuliza, wengi hawajui wanapataje majibu ya maswali yao.

Vijana kuna mahali wanatamani kufika kiuchumi, kihuduma, kisiasa nakadhalika.

Habari njema ni kwamba "majibu ya maswali ya vijana yanapatikana kwenye neno la Mungu - kwa Mungu"

Jambo ambalo shetani amelifanya kwa vijana ni kuwatenganisha vijana na neno la Mungu.

Vijana wengi hawasomi na hawajifunzi neno la Mungu, hawajihudhurishi kwenye mafundisho ya neno la Mungu.

Shetani anajua akiwatenganisha na neno la Mungu, vijana watapoteza muelekeo na maisha yao yataharibika.

Wahanga wengi wa utandawazi ni vijana, wahanga wengi wa mapenzi ni vijana ndio maana utasikia wengine wamechoma moto wapenzi wao, wamewapiga risasi wapenzi wao nakadhalika, ndoa za vijana sikuhizi hazidumu, watoto wanaolelewa na mzazi mmoja wameongezeka, vijana hawataki kuoa, vijana wanaotelekezwa na mimba wamekuwa wengi, tatizo kubwa ni kwamba VIJANA WAMEACHANA NA NENO LA MUNGU LENYE MAJIBU YA CHANGAMOTO NA MASWALI YAO.

WITO KWA KWA VIJANA

●Usalama wenu ni neno la Mungu, rejeeni kwenye neno la Mungu.

●Kama hauna Biblia, nunua Biblia.

●Kama unayo na hausomi, anza kuisoma sasa.

●Neno la Mungu ni taa na mwanga wa njia yako.

Chapisha Maoni

0 Maoni