UMUHIMU WA KUWEKEZA KWA VIJANA ILI KUTENGENEZA TAASISI IMARA

 


(Danieli 1:1-5)

 UTANGULIZI

Kuna taasisi nyingi hapa ulimwenguni kama vile serikali, ndoa, shule, vyuo, majeshi nakadhalika.

 Vijana ni kundi muhimu sana katika ujenzi wa taasisi yoyote endapo uwekezaji mkubwa utafanya katika kundi hili.

 MFALME NEBUKADNEZA

Alifanya uwekezaji kwa vijana kwa muda miaka mitatu, vijana ambao walitakiwa kufanya kazi mbalimbali katika jumba la Mfalme.

 Baadhi ya maeneo ambayo Mfalme Nebukadneza aliwekeza kwa vijana;-

 1.  Aliwekeza ili vijana wapate elimu.

·      2. Aliwekeza kwenye afya za vijana hao, kwa muda wa miaka mitatu vijana walikuwa wanakula kutokana na bajeti ya Mfalme Nebukadneza.

 BAADHI YA SABABU KWA NINI TUWEKEZE KWA VIJANA

1.     Vijana wana nguvu.

2.     Vijana ni wepesi wa kujifunza mambo mbalimbali.

3.     Miili ya vijana inaweza kustahimili mazingira ya aina mbalimbali.

 

HITIMISHO

Tukitaka kutengeneza taasisi zenye uimara endelevu hatupaswi kuogopa au kuepuka kuwekeza kwa vijana.

Chapisha Maoni

0 Maoni