✍Faraja Gasto
Mungu huwapa watu nafasi za aina mbalimbali na kwa malengo mbalimbali.
Kuna nafasi ambazo Mungu huwapa watu kimkakati (nafasi za kimkakati) kwa ajili ya kusudi fulani, nafasi katika serikali, katika jamii, katika taasisi nakadhalika.
BAADHI YA MIFANO YA WATU WALIOPEWA NAFASI ZA KIMKAKATI
● Malkia Esta (Esta 4:14-17)
Mungu alimpa Esta nafasi ya umalkia kwa ajili ya usalama wa Wayahudi.
Lilipozuka jambo baya kinyume na wayahudi, watu walimuombea Esta akatumiwa na Mungu kuwaokoa Wayahudi wasiangamizwe na Hamani.
●Yusufu (Mwanzo 45:6-7)
Mungu alimpa Yusufu nafasi katika serikali ya Misri lengo mojawapo ni kwa ajili ya kuhifadhi familia yake na kuuingiza uzao wa Ibrahimu kwenye nchi ya ugeni kama Mungu alivyosema uzao wa Ibrahimu utakwenda ugenini (Mwanzo 15:13).
VITA VYA WATU WENYE NAFASI ZA KIMKAKATI
●Shetani huwapiga vita ili wasikae kwenye nafasi hizo.
●Shetani hutumia hofu kuwazuia wasilitimize kusudi la Mungu (Esta 4:11) shetani alihakikisha Esta anajawa na hofu ili asilitimize kusudi la Mungu.
NAMNA YA KUWAOMBEA WATU WENYE NAFASI ZA KIMKAKATI
●Omba Mungu awape kutambua ni yeye amewapa nafasi hizo. Mordekai alimjulisha Esta kwamba nafasi hiyo Mungu alimpa kwa ajili ya wayahudi (Esta 4:14)
●Omba Mungu awavike nguvu za kulitimiza kusudi lake kupitia nafasi hizo.
●Omba Mungu awaondolee hofu.
●Omba Mungu awalinde awaokoe na hila za waovu, Biblia inasema Danieli alitengenezewa kesi na akatupwa kwenye tundu la Simba ili aachie ile nafasi aliyokuwa nayo lakini Mungu alimwokoa (Danieli 6:1-25).
0 Maoni