MAMBO YATAKAYOWASAIDIA VIJANA KUTOYAAMSHA NA KUTOYACHOCHEA MAPENZI


(Wimbo ulio bora 2:7)

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.

Ushauri wa hekima alioutoa Mfalme Sulemani kwa binti au wanawake wa Yerusalemu unatupa ufahamu huu;-

●Mapenzi yamo ndani ya mtu ndio maana anasema msiyaamshe na msiyachochee.

●Mapenzi yanaweza kuamshwa na kuchochewa.

●Kuna mambo yanayoweza kusababisha mapenzi yakaamka au kuchochewa.

●Mapenzi yana wakati wake sahihi wa kuamka au kuchochewa.

●Mapenzi huwa yanajiamsha yenyewe ukifika wakati wake.

●Kuna madhara ya kuyaamsha na kuyachochea mapenzi kabla ya wakati wake ndio maana anawashauri wasiyachochee na kuyaamsha.

●Wahanga wakubwa wa mapenzi ni wanawake ndio maana anaelekeza ushauri kwa wanawake sio wanaume.

Niishie hapo nieendelee na mengine.

KWA NINI USIYAAMSHE AU KUYACHOCHEA MAPENZI KABLA YA WAKATI WAKE? (Huyu sio Roho ni mimi, nami naamini nina Roho wa Mungu 🤣🤣🤣)

●Ili kuzuia mimba zisizotarajiwa.

●Ili kulinda maadili ya jamii, binti akijiingiza kwenye mapenzi kabla ya wakati ni rahisi kutumbukia kwenye uhuni labda ule mkono uliomshika Mtume Petro asizame umuokoe.

●Ili kulinda afya na miili ya wanawake, wataalamu wanasema binti akijiingiza kwenye mapenzi mapema au akizaa akiwa na umri chini ya miaka kumi na nane anajiweka kwenye hatari mbalimbali.

Niishie hapo nieendelee na mengine.

WAKATI SAHIHI WA KUYAAMSHA NA KUYACHOCHEA MAPENZI NI UPI? (Huyu sio Roho ni mimi, nami naamini nina Roho wa Mungu 🤣🤣🤣)

●Wakati ukiwa tayari kuoa na kuolewa.

●Wakati ukiwa na uwezo wa kumudu gharama za mapenzi.

--》Mapenzi ni gharama, mapenzi yalimfanya Yesu akafa msalabani, jiulize haya machache je! huyo mkaka au mdada figo zake zikifeli utamgawia figo moja? je! una mahari za kumtolea huyo mdada? je! huyo mkaka au m'baba akipatwa na misukosuko utasimama naye au utajiunga na chama cha mke wa Ayubu (Ayubu 2:9)

Niishie hapo niendelee na mengine.

MAPENZI YAKO YAAMSHE NA UYACHOCHEE KWA WATU HAWA

●Mume aliyekuoa.

●Mke uliyemuoa.

Angalizo: uchumba sio ndoa hivyo basi usiyaamshe mapenzi kwa mchumba, uchumba  ukifa usije kutusumbua na posts zako za kuomba ushauri na kututaka tukutie moyo 😂😂😂😂😂

MAMBO YATAKAYOWASAIDIA VIJANA KUTOYACHOCHEA AU KUYAAMSHA MAPENZI 

Kuna funguo mbili za kuyaamsha na kuyachochea mapenzi, funguo hizo ni UFAHAMU NA HISIA, hivyo basi;-

●Epuka kutazama picha, video na kusikiliza maneno yanayozungumzia mapenzi.

●Epuka kuzungumzia mambo ya mapenzi, kutumiana jumbe za mapenzi, kukaa kwenye mabaraza yanayozungumzia mapenzi nakadhalika.

●Epuka kukaa na watu wanaojihusisha na mapenzi.

●Epuka kutazama watu waliovaa nusu uchi.

●Kemea roho chafu zinazoamsha mapenzi ndani yako na usizipe nafasi roho chafu zinazoamsha mapenzi kwa kuepuka kutafakari mapenzi, mwili wa mkaka au mdada, epuka kusikiliza na kutazama mambo ya mapenzi.

●Epuka kushikwashikwa na kushikanashikana katika namna isiyo salama.

Niishie hapa.


Chapisha Maoni

0 Maoni