MTUMISHI NA TABIA YA MTUMISHI


✍Faraja Gasto

1 Wathesalonike 1:5

"ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa TABIA ZETU kwenu, kwa ajili yenu".

Jambo mojawapo lililochangia mafanikio ya huduma ya Mtume Paulo na watenda kazi wenzake ni TABIA ZAO (TABIA ZAO NJEMA)

Kuna watu ni watumishi wa Mungu wazuri kabisa wana upako, neema, maarifa ya rohoni nakadhalika lakini HAWANA TABIA NZURI.

Wapo ambao wana tabia ya kupenda fedha, ukorofi, waongo, midomo michafu,  wasiojali wengine, wanaopenda kujipendekeza kwa serikali nakadhalika.

Kila mtumishi wa Mungu anapaswa kufahamu kuwa tabia yake ina mchango mkubwa katika kudumaa, kufanikiwa na kusitawi kwa huduma yake hivyo basi kila mtumishi anapaswa KUBORESHA TABIA YAKE.

Ni vizuri kila mtumishi awe na muda wa kujifanyia tathmini kuhusu namna anavyoenenda ili aone kama kuna tabia isiyo nzuri aanze kukabiliana nayo.

Ni kweli kabisa mabadiliko ya kitabia huchukua muda hivyo basi tunapojigundua tuna tabia isiyo nzuri ni vizuri kuchukua hatua ya kukabiliana na tabia hizo.

NB: 

●Kutumiwa na Mungu haimaanishi una tabia nzuri.

●Mungu anaweza kukutumia hata kama tabia zako sio nzuri ila tabia zisizo nzuri zinaweza kukusababishia matatizo mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni