Zipo tabia nyingi sana za watu makini, tabia mojawapo ya watu makini ni KUJITAFUTIA USAHIHI WA MAMBO kabla ya kuandika, kusema nakadhalika.
Luka 1:3
"nimeona vema mimi nami, kwa kuwa NIMEJITAFUTIA USAHIHI WA MAMBO hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu"
Usahihi wa mambo maana yake una ushahidi wa kutosha, rejea za kutosha na ushahidi usio na dosari kuhusu jambo au mambo fulani.
Usahihi wa mambo unatokana na tafiti, shuhuda, ushahidi, historia nakadhalika.
NB: Unaweza kuamua kuwa miongoni mwa watu makini kwenye hii sayari ya dunia ikiwa utajifunza kuwa mtu makini.
0 Maoni