NAMNA YA KUTUNZA FEDHA AU HAZINA

 


(MATHAYO 6:19-21)

JAMBO LA KWANZA: WEKA MAHALI AMBAPO HAUWEZI KUICHUKUA KWA HARAKA AU KUPAFIKIA KWA HARAKA

Kwa mfano Yesu alisema tuweke hazina mbinguni, mbinguni huwezi ukapafikia kirahisi na kwa kuwa huwezi kupafikia kirahisi basi hauwezi kuchukua kirahisi.

JAMBO LA PILI: WEKA MAHALI AMBAPO SIO RAHISI KUHARIBIKA

Usiweke fedha ardhini, usiweke mahali ambapo wanayama kama vile panya wanaweza kuzifikia fedha na kuzila.

Bibilia inasema ukiweka mbinguni nondo au kutu hawawezi kuharibu, hiyo inatupa picha kuwa fedha au hazina haipaswi kutunza mahali ambapo inaweza kuharibiwa.

JAMBO LA TATU: WEKA MAHALI AMBAPO SIO RAHISI MTU KUIBA

Yesu anasema tuweke hazina mbinguni kwa kuwa huko wezi hawawezi kuvunja na kuiba, hiyo inatupa picha kufahamu kuwa mahali tunapopaswa kuweka fedha au hazina ni mahali ambapo sio rahisi mtu kuiba.

JAMBO LA NNE: FICHA FEDHA AU HAZINA

Yesu anasema tuweke hazina mbinguni, mbinguni pamefichika hapaonekani kwa urahisi. Hiyo inatupa pcha kufahamu kuwa fedha au hazina zinapaswa kufichwa, hazina haipaswi kuwa mahali panajulikana kwa kila mtu (Isaya 45:1-3)(Mathayo 13:44)

Chapisha Maoni

0 Maoni