Lengo la somo: kukusaidia kutathmini ikiwa umekua kiroho au kukusaidia kutathmini ikiwa mtu Fulani au watu Fulani wamekua kiroho.
ISHARA YA KWANZA: UWEZO WA KUMSIKIA MUNGU NA KUIJUA SAUTI YA MUNGU
(1 Samweli 3:1-10) Samweli alisikia sauti ya Mungu lakini alishindwa kujua kama ile sauti ni ya Mungu akadhani ni sauti ya kuhani Eli. Wapo watu ambao hawaiskii sauti ya Mungu kwa sababu mbalimbali pia wapo wanaosikia sauti ya Mungu na hawajui kama ni sauiti ya Mungu. Mtu aliyekua kiroho anasikia na anaweza kupambanua sauti ya Mungu na sauti zingine.
ISHARA YA PILI: UWEZO WA KUPAMBANUA MEMA NA MABAYA
Kwenye hii dunia kuna mambo huwa yanakuja kama mema kumbe ni mabaya na kuna mambo huwa yanakuja kama mabaya kumbe ni mema. Mtu aliyekua kiroho anaweza kupambanua mema na mabaya haijalishi yamekuja kwa namna gani (Waebrania 5:13-14)
ISHARA YA TATU: KUISHI KWA IMANI
Kuishi kwa imani ni kuishi kwa kusikia sauti ya neno la Mungu (Warumi 10:17). Mtu aliyekua kiroho anaweza kuishi kwa imani.
ISHARA YA NNE: KUYATAFUTA, KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU NA KUYATENDA
Mtu aliyekua kiroho hutaka kuyajua mapenzi ya Mungu katika mambo mbalimbali na kutenda sawasawa na mapenzi ya Mungu (Yohana 4:34)
ISHARA YA TANO: KUONDOKANA NA TABIA YA MWILINI NA KUWA NA TABIA YA ROHONI
(1 Wakorintho 3:1-9)(Wagalatia 5:19-21) mtu aliyekua kiroho hana tabia ya mwilini bali ana tabia ya rohoni.
0 Maoni