(Kumbukumbu la torati 28:1-14)
UTANGULIZI
Mungu ni Mungu aliye hai, Mungu huongea na watu hata sasa kwa njia mbalimbali kama vile kwa njia ya ndoto, maono, ishara, kupitia watu, ndani ya moyo wa mtu nakadhalika. Shida waliyonayo watu wengi ni kutoitambua sauti ya Mungu (1 Samweli 3:18)
NAMNA MUNGU ANAVYOONGEA MOYONI
1. 1. Mungu huweka neno katika moyo wa mtu (Nehemia 2:12)(Luka 15:17)
2. 2. Moto moyoni (Matendo 2:37)(2 Samweli 24:10)
3. 3 . Amani ya Kristo (Wakolosai 3:15) wakati Fulani nilikuwa namuomba Mungu jambo fulani, wakati naendelea kuomba Mungu aliachilia amani yake ndani yangu nikajua tayari Mungu ametenda kisha nikaacha kuomba, baada ya siku si nyingi Mungu alinipa nilichoomba.
4. 4. Wazo au mawazo (Isaya 55:8)
5. 5. Msukumo Fulani moyoni (Esta 6:1-12) Mfalme aliwekewa msukumo wa kusoma kitabu, Mungu alitaka Mfalme aone habari za Mordekai
6. 6. Ujasiri (Isaya 1:6-7) Ujasiri unaotoka kwa Mungu hukufanya ufanye mambo yasiyo kinyume na neno la Mungu
7. 7. Mzigo moyoni (Mathayo 11:30) Wengine huwekewa mzigo wa kuomba, kuombea, kutoa sadaka au kufanya jambo Fulani
8. 8. Huruma (Luka 7:11-15)
9. 9. Bidii (2 Wakorintho 8:16) kuna wakati Mungu huachilia bidii ndani ya mtu ili afanye jambo Fulani
BAADHI YA VIKWAZO VYA KUMSIKIA MUNGU MOYONI
1. 1. Ugumu wa moyo (Waebrania 3:15)
2. 2. Kukosa neno la Mungu moyoni (Wakolosai 3:16) Daudi alisema (Zaburi 119:11)
HITIMISHO
Kumsikia Mungu na kumtii ndio chanzo cha Baraka za Mungu, amani nakadhalika, lakini kitu cha msingi ni kusikia ndio maana Mungu anasema “itakuwa utakaposikia” (Kumbukumbu la torati 28:1-14)
0 Maoni