UHUSIANO WA MABADILIKO YA TABIA ZA WANADAMU NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

✍️✍️Faraja Gasto

(Zaburi 107:34)

Lengo la makala hii: kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa mbinu za kibiblia.

Utangulizi

Mabadiliko ya tabia ya nchi ni mojawapo ya matatizo yanayosumbua dunia, tatizo hili limeleta athari si kwa wanadamu tu bali hata kwa viumbe wengine waliopo duniani.

Katika kitabu cha zaburi 107:34 Biblia inatupa kufahamu kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mabadiliko ya tabia ya nchi na mabadiliko ya tabia za wanadamu, Biblia inasema “nchi ya matunda mengi ikawa uwanda wa chumvi kwa sababu ya ubaya wao walioikaa”

Kwa hiyo tabia zetu wanadamu zinaweza kusababisha mambo mbalimbali kutokea ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi.

Hitimisho

Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kila mtu anapaswa kuishi sawasawa na neno la Mungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni