✍️✍️ Faraja Gasto
Utangulizi
Mungu huwapa watu
1.Kazi
2.Mali
3.Fedha n.k
4.Elimu nakadhalika
Mungu anapompa mtu kitu au fursa anakuwa na sababu fulani kwa mfano
1.Nehemia (Nehemia 1:1-11, 2:1-8)
Mungu alimpa nafasi ya kufanya kazi ikulu kwa Mfalme Ahasuero sio kwa sababu Nehemia apate pesa tu bali ilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa kuta za Yerusalemu.
2.Yusufu Mwanzo 15:13-16)
Mungu alimpa Yusufu nafasi ya kazi kwa Mfalme Farao sio kwa sababu Yusufu apate pesa tu bali bali afanyike mlango wa kuliingiza taifa la Israeli katika nchi ya Misri kwa kuwa Mungu alimwambia Ibrahimu uzao wako utakaa Misri kwa muda miaka mia nne (Mwanzo 15:13-16)
3.Esta (Esta 4:12-14)
Mungu alimpa Esta nafasi ya umalkia ili awe sababu ya wayahudi kutoangamizwa kutokana na mpango wa Hamani
4.Obadia (1 Wafalme 18:3-4)
Mungu alimpa Obadia nafasi kwenye ikulu ya Mfalme Ahabu ili ahudumie maisha ya watumishi wa Mungu
5. Danieli, Shadraka, Meshaki na Abednego (Danieli 1:3-5)
Mungu aliwapa nafasi ya kusoma na kufanya kazi kwenye ufalme wa Mfalme Nebukadneza wakina Danieli, Shadraka, Meshaki na Abednego ili Babeli yote ijue kuna Mungu ambaye ni zaidi ya miungu inayoabudiwa pale Babeli. Danieli ndiye alitafsiri ndoto ya Mfalme Nebukadneza hiyo ndoto iliwashinda wachawi, kutokana na imani ya wakina Shadraka, Meshaki na Abednego moto haukuwateketeza hatimaye Mfalme Nebukadnze akakiri hakuna Mungu kama Mungu wa vijana hao.
6. Mnyweshaji wa Mfalme (Mwanzo 40:1,9-15,20-23, 41:9-40)
Mungu alimjalia mnyweshaji wa Mfalme kurejea kwenye nafasi yake si kwa ajili ya faida yake mwenyewe bali kwa ajili ya kuinuliwa kwa Yusufu.
HITIMISHO
Mungu anapokupa kazi, fedha, elimu, mali nakadhalika usidhani ni kwa ajili yako tu au usidhani ni kwa ajili ya faida yako tu bali kuna kusudi la Mungu hivyo basi ni muhimu utake kufahamu nini ni sababu ya Mungu kukupa elimu, kazi, mali, fedha nakadhalika.
Ni wengi wanataka kazi hawajapata na wana elimu kubwa lakini wewe umepata ujue kuna kusudi la Mungu.
Ni wengi wanatafuta fedha lakini hawajazipata wanazotaka ila wewe umepata mianya ya fedha ujue kuna kusudi la Mungu.
0 Maoni