✍️✍️✍️Faraja Gasto
UTANGULIZI
Duniani kuna aina ya watu ambao maneno yao yana nguvu kutokana na sababu mbambali kwa mfano kuna wazazi wanawalaani watoto wao na laana hizo zinawapata, kuna viongozi wakisema neno linatimia au linatekelezwa kutegemeana na nafasi zao za uongozi.
Kwa mfano Nabii Eliya alisema “mvua haitanyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu na ikawa hivyo” (1 Wafalme 17:1)
Kwa mfano akida alisema neno lake lina mamlaka kwa askari walio chini yake (Luka 7:8)
Mambo yatakakusaidia ili maneno yako yawe na nguvu
✓Jitambue kama mtumishi wa Mungu (Isaya 44:26)
Mungu huyathibitisha maneno ya watumishi wake, ndio maana Nabii Eliya alisema mvua haitanyesha isipokuwa kwa neno langu na Mungu akathibitisha mvua haikunyesha (1 Wafalme 17:1)
✓Itambue nafasi yako katika ulimwengu wa roho
Nafasi zina mahusiano na nguvu ya maneno kwa mfano neno la Mfalme ni sheria, neno la Rais lina nguvu kutokana na nafasi yake, anapotamka jambo mamlaka zinaanza kutekeleza neno lile kwa kuwa limetamkwa na mtu aliye kwenye nafasi fulani.
Ndivyo ilivyo kwetu sisi wakristo, kila aliyemwamini Yesu anapaswa kufahamu kuwa ana nafasi kubwa sana katika ulimwengu wa roho, kila aliyeokoka AMEKETISHWA PAMOJA NA KRISTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (Waefeso 2:6)
✓Tamka kwa imani (Marko 11:12-14,20-23)
Yesu aliuambia mtini “watu wasile matunda kwako” kesho yake wanafunzi walikuta mti umekauka
Yesu alitufunulia siri kuhusu namna imani inavyoweza kusababisha maneno yetu yawe na nguvu, Yesu alisema “ATAKAYEUAMBIA mlima huu ng'oka ukatupwe baharini na asione shaka moyoni mwake itakuwa hivyo”
0 Maoni