(Isaya 44:6)(Ufunuo 1:8)
UTANGULIZI
Kuna aina mbalimbali za majina kwa mfano majina ya viumbe, majina ya vitu, majina ya maeneo pia kuna majina ya kazi kama vile askari, daktari, Rais, Mfalme nakadhalika
Pia Mungu anayo majina mengi ya kazi kwa mfano Bwana wa majeshi, Mfalme wa amani, mhukumu wa haki, mwanzo na mwisho nakadhalika.
Maana kadhaa ya mwanzo na mwisho
1.Anaweza kuanzisha jambo na kulifikisha mwisho
Kwa mfano yeye Mungu ndiye mwanzo wa uhai, yeye ndiye aliumba kila unachokiona na usichokiona (Yohana 1:1-3)
2.Anaweza kumpa mtu mwanzo au pa kuanzia
Kwa mfano kuna wengine wanataka waende mahali fulani au wafanye jambo fulani lakini hawajui waanzie wapi, Mungu anaweza kuwapa mahali pa kuanzia, anaweza akawapa mbinu za kuanzia naadhalika.
Kwa mfano Mungu alipomuita Gideoni akawaokoe waisraeli kutoka kwenye utumwa wa wakaani alimwambia mahali pa kuanzia (Waamuzi 6:14,25)
3. Anajua kupanga mambo yanayopaswa kuanza na yanayopaswa kuwa mwisho
Kwa maana nyingine ni kwamba Mungu anajua kuweka vipaumbele, kipi kianze na kipi kiwe cha mwisho kwa mfano Biblia inasema “hapo mwanzo aliziumba mbingu na nchi” maana yake ni kwamba kitu cha muhimu zaidi katika uumbaji kilikuwa ni mbingu na nchi (Mwanzo 1:1).
4. Anaweza kukuambia mwisho wa jambo litakavyokuwa hata kabla haujalianza
(Isaya 46:10)
Hitimisho
✓Kuna jambo umekuwa unataka ulifanye na haujui uanzie wapi?
✓Kuna mahali unatamani kwenda na haujui unanzie wapi?
✓Kuna jambo unatamani kulizungumza na haujui unazie wapi?
✓Basi majibu utayapata kwa Mungu aliye alfa na omega.
0 Maoni