Faraja Gasto ✍️✍️✍️
Ikiwa uliwatendea watu mema halafu wema wako ukasahaulika au wema wako ukaonekana si kitu USIHUZUNIKE WALA USINUNG'UNIKE.
Wanadamu wanaweza kusahau wema uliowatendea lakini MUNGU HASAHAU.
Mordecai alibaini mpango mbaya wa kumwua Mfalme Ahasuero kisha akatoa taarifa kwa Malkia kisha Malkia akamjulisha Mfalme, uchunguzi ulipofanywa ikabainika ni kweli walinzi wawili wa milango ya vyumba vya Mfalme walikusudia kumuua Mfalme Ahasuero , watu hao wakauawa (Esta 2:21-23) lakini wema huo wa Mordekai haukumpa faida yoyote kwa wakati huo isipokuwa wema huo uliandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu.
Baada ya muda fulani Mungu alihakikisha Mordekai anapata faida ya wema aliomtendea Mfalme Ahasuero (Esta 6:1-10)
KWA NINI NIMEKUTAZAMISHA HAYO?
Ili kukutia moyo kuwa wanadamu wanaweza kusahau wema uliowatendea lakini MUNGU HASAHAU, ipo siku Mungu atahakikisha unapata faida ya wema uliowatendea watu.
HITIMISHO
Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho (Wagalatia 6:9)
0 Maoni