KUILIMA NA KUITUNZA:UJUMBE KWA WANAUME WALIOOA


Faraja Gasto ✍️✍️✍️✍️

---KULIMA NA KUTUNZA----


(Mwanzo 2:15)


Mungu alimuweka Adamu kwenye bustani ya Edeni huku akiwa na jukumu la Kulima na kutunza bustani.


KULIMA - Kuitumia ardhi ya bustani kwa manufaa yake.


KTUNZA - Kuhakikisha ardhi iko vizuri kwa matumizi endelevu.


KATIKA NDOA IKO HIVI

KULIMA - ni kumtumia mwanamke kukidhi haja ya mwili (tendo la ndoa)


KUTUNZA - Kuhakikisha unayemtumia unamtunza ili aendelee kukuvutia kumtumia tena na tena.


TATIZO MOJAWAPO LA WANAUME WENGI


Ni kumtumia mwanamke au kuwatumia wanawake bila kuwatunza, kutokana na kutokuwatunza wake zao ndio maana wanaume wengine huanza kuona wake zao wamepoteza mvuto na hili limepelekea wengine kuwa na masuria (Hawara)


NB: Yapo mambo mengi yanayopelekea wanaume kuwa na masuria, jambo mojawapo ni wake zao kupoteza mvuto kutokana na kutotunzwa.


HITIMISHO

Wanaume tunzeni wake zenu, bidii mliyonayo ya kuwatumia, hiyo bidii iwe katika kuwatunza pia ili waendelee kuvutia kwa matumizi endelevu.

Chapisha Maoni

0 Maoni