KUFAHAMU NENO ALILONALO MUNGU KWA AJILI YAKO KATIKA NYAKATI MBALIMBALI


 ✍️Faraja Gasto


UTANGULIZI

Mungu anapotaka kufanya kazi mbalimbali hapa duniani hutumia njia mbalimbali ikiwemo NENO LAKE (Rejea, Isaya 55:8)(Zaburi 107:20). Mungu hutumia neno lake kuponya, kuokoa, kutenda miujiza, kutia moyo, kufundisha, kubadilisha watu, mazingira, mifumo nakadhalika, Mungu hutumia neno lake kuongoza watu, kuinua watu,  kuonya watu, kupatanisha watu nakadhalika.


Mungu analo neno kwa ajili ya kila mtu katika nyakati zote (wakati wa mafanikio, wakati wa majaribu, wakati ukiwa umechoka, umekata tamaa, umerudi nyuma, umekwazika, umekwaza mtu, unapojeruhiwa, unapojeruhi nakadhalika)


SOMA MIFANO HII 

✓Mungu alikuwa na neno kwa ajili ya Zerubabeli (Zekaria 4:6)


✓Wakati Kaini alipoghadhibika, Mungu alikuwa na neno kwa ajili ya Kaini (Mwanzo 4:6-7)


✓Ukisoma habari za yale makanisa Saba yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana utaona Mungu akisema "YEYE ALIYE NA SIKIO ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA" (Ufunuo wa Yohana 2:7,11,17,26)(Ufunuo wa Yohana 3:6, 13,22)


Hiyo ni baadhi ya mifano inayotuwezesha kufahamu kuwa Mungu analo neno kwa ajili ya kila mtu katika nyakati zote.


BAADHI YA MBINU ZITAKAZOKUSAIDIA KUFAHAMU NENO ALILONALO MUNGU KWA AJILI YAKO

1.Jenga tabia ya kuwa na faragha na Mungu kwa njia ya maombi.


2. Soma neno la Mungu.


3.Msikilize Roho Mtakatifu aliye ndani yako (ikiwa umemwamini Yesu).


4. Jenga tabia ya kutaka kufahamu Mungu ana neno gani kwa ajili yako kwa kumuuliza. Yoshua aliuliza Je! Bwana amwambia nini mtumishi wake akaambiwa avue viatu vyake (Yoshua 5:13-15)



HITIMISHO

Ni muhimu sana kufahamu neno alilonalo Mungu kwa ajili yako katika kila nyakati.

Chapisha Maoni

0 Maoni