Ni rahisi sana kupata nyumba ya ibada na ukaanza kwenda kuabudu humo/hapo au ukawa mshirika.
Ila usidhani ni rahisi kupata Mchungaji (mtu wa kukuchunga ambaye atatimiza wajibu wake wa kuhakikisha unatembea katika njia za Mungu, ambaye atakukemea ukienda kinyume na neno la Mungu bila kujali hadhi yako ya kikazi, kiuchumi nakadhalika, ambaye atakutia moyo, ambaye anajua ipo siku atatoa hesabu kwa Mchungaji Mkuu Bwana YESU, ambaye atalipa gharama za aina mbalimbali ili uwe salama, ili ujengwe, uimarike, usitawi nakadhalika.
Hivyo basi unapofanya maamuzi kuhusu wapi uwe mshirika usitazame jengo la ibada, umaarufu wa dhehebu, ibada zinaendeshwa kwa lugha ya kihindi, kingereza, kichina, kifaransa nakadhalika, usiende kwa sababu umeona wadada au wakaka wamekuvutia hapo kwenye nyumba ya ibada, vitu vinavyoonekana kwa macho ya kimwili nakadhalika.
Hakikisha unapata Mchungaji kwa kuwa ni heri uwe na Mchungaji ambaye anafanyia huduma chini ya mti au nyumbani kwake au shuleni au kwenye ukumbi nakadhalika kuliko kuwa kwenye jengo zuri la ibada lenye viyoyozi halafu hauna Mchungaji.
NB: Mchungaji ni mtu wa muhimu sana kwenye maisha yako, hakikisha unapata Mchungaji.
0 Maoni