UTANGULIZI
Kila mwandamu hupatwa na nyakati ngumu, nyakati ambazo mtu hujikuta amekata tamaa, amepoteza matumaini, anaona kama duniani yuko peke yake hakuna wa kumsaidia, nyakati ambazo mtu anaona giza limetanda, hofu imetanda nakadhalika.
Wengine wanapopatwa na nyakati hizi hujikuta wameharibikiwa zaidi, wengine hufanya maamuzi ambayo sio mazuri ikiwemo kujiua nakadhalika.
Ili upite salama katika nyakati hizi yapo mambo ya kufanya yanayofundishwa na Biblia, katika somo hili tutajifunza mambo mawili tu.
MAMBO YA KUFANYA
1.MAOMBI
Nataka tuone mifano ifuatayo ili tujifunze
Mfano wa 1: Wayahudi waliponusurika kuuawa
(Esta 3:5-6,4:15-16)
Ilifika hatua Wayahudi wakajikuta kwenye wakati mgumu sana kutokana na mpango wa kuwaangamiza.
Wayahudi walimuombea Malkia Esta ili akazungumze na Mfalme, Yale maombi yalipelekea kubadilika Kwa mpango ule hatimaye Wayahudi wakabaki salama.
Mfano wa 2: Bwana Yesu
(Marko 14:32-41)
Ulifika wakati Bwana Yesu alijikuta kwenye wakati mgumu, akawaambia wanafunzi wake "nina huzuni nyingi kiasi cha kufa"
Bwana Yesu alipokuwa kwenye wakati huo mgumu alimuomba Mungu (Baba yake)
NB: Maombi yanaweza kukusaidia kuvuka salama kwenye nyakati ngumu.
2.KUFUATA MAELEKEZO YA MUNGU
Nataka tutazame mifano hii michache
Mfano wa 1: Maelekezo ya Mungu kwa Gideoni
(Waamuzi 6:1-27)
Wana wa Israeli walijikuta kwenye wakati mgumu sana kutokana na utumwa.
Walipomlilia Mungu wao, Mungu alipitisha maelekezo Kwa Gideoni kuhusu namna watakavyotoka kwenye utumwa.
Gideoni alipotendea kazi maelekezo ya Mungu, maisha ya wana wa Israeli yalibadilika.
Mfano wa 2: Maelekezo ya Mungu kwa Musa
(Kutoka 3:7-22)
Wana wa Israeli walikuwa kwenye utumwa mzito, maisha yao yalikuwa magumu sana, Mungu alimpa Musa maelekezo ya namna wana wa Israeli watatoka kwenye nchi ya Misri ambayo ilikuwa nyumba ya utumwa.
NB: Maelekezo ya Mungu yanaweza kukuvusha kwenye nyakati ngumu.
0 Maoni