✍️Faraja Gasto
Somo hili lina sehemu kuu mbili
✓Baadhi ya misingi ya MAOMBEZI
✓Mambo ya kuzingatia katika MAOMBEZI
UTANGULIZI
Maombezi ni ya muhimu sana Kwa kuwa yaharibu na kuvunja kazi za shetani, yanasaidia katika kutatua matatizo mbalimbali nakadhalika.
BAADHI YA MISINGI YA MAOMBEZI
✓MAHUSIANO NA MUNGU
Ili maombezi yawe na ufanisi lazima anayeombea awe na mahusiano mazuri ya anayeombwa (Mungu).
Wana wa Askofu Skewa walijaribu kukemea Pepo lakini Pepo hakutoka kwa kuwa hao watoto wa Askofu hawakuwa na mahusiano mazuri na Mungu (Matendo ya mitume 19:13-17)
Maombi ya Musa kwa ajili ya wana wa Israeli yalikuwa na ufanisi Kwa kuwa Musa alikuwa na mahusiano mazuri na Mungu (Kutoka 32:7-14)
✓IMANI NA NENO LA MUNGU
Anayeombea na anayeombewa lazima wawe na imani kwa sababu bila imani hakuna kinachoweza kutokea (Marko 11:24-25)(Mathayo 15:28)
Imani huja kwa kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17), Kwa hiyo anayeombewa ni muhimu afundishwe neno la Mungu ili kujenga imani ndani yake ili akiombewa apokee anachoombewa.
✓ROHO MTAKATIFU
Ni muhimu kumpa nafasi Roho Mtakatifu aongoze maombezi kwa kuwa yeye ndiye anajua mambo yote (yaliyopita, yaliyopo na yajayo) hata mambo ya Siri.
(Warumi 8:9,14)
Hatupaswi kutegemea akili zetu katika kuwaombea watu lazima tukubali kumpa nafasi Roho Mtakatifu aongoze maombezi.
BAADHI YA MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAOMBEZI
1.KUJUA HISTORIA YA TATIZO LA ANAYEOMBEWA
Yesu alimuuliza baba yake na mtoto mwenye Pepo kifafa je! huyu mtoto amekuwa hivi tangu lini? (Marko 9:20-21)
2.MAZINGIRA YA ANAYEOMBEWA
-Kama anayeombewa Yuko hospitali ni vema kuomba kwa sauti ndogo.
-Kama amesimama ni vema wawepo watu nyuma yake ili ikitokea Pepo wakamtoka akianguka asiumie.
-Kama uayemuombea Yuko ghorofani hakikisha yuko mahali ambapo hata kama itatokea pepo wakalipuka, mtu huyo hataangukia mahali patakaposababisha madhara.
3.KUWEKEA MIKONO
(Marko 16:18)(Marko 8:23-25)
Katika kuwawekea watu mikono ni muhimu sana mtu apige magoti ili anayeombea asije akamdondoshea mate anayeombewa.
Kama mtu anayeombewa amesimama ni vema anayeombea asimame katika namna ambayo mate yanayotoka kinywani mwa anayeombea hayatamgusa anayeombewa.
4.MUENDELEZO WA MAOMBI
(Marko 8:22-26)
Yesu alipomgusa mara ya kwanza kipofu hakuona vizuri, Yesu akamgusa mara ya pili ndipo kipofu akaona vizuri.
(2 Wafalme 4:32-37)
Nabii Elisha alipomgusa mtoto mara ya kwanza mwili ukianza kupata moto lakini mtoto hakufufuka lakini akaendelea kuomba Kisha akamgusa tena ndipo mtoto akafufuka.
Kama umemuonbea mtu mara ya kwanza na hakuna kilichotokea endelea kumuombea (unaweza kumuombea wakati huohuo au wakati mwingine)
5.MTAZAME MTU USONI AU MWAMBIE MTU AKUTAZAME USONI.
–Macho huwa yanaongea
–Macho huwa yanapitisha vitu kutoka kwa mtu mmoja kwenda Kwa mwingine.
Elima mchawi alikuwa akiachia uchawi kupitia macho yake ili kumfanya Sergio Paulo asiamini injili (Matendo ya mitume 13:6-8)
Mtume Paulo alipotaka kumshughulikia Elima mchawi alimkazia macho (Matendo ya mitume 13:9-11)
Mtume Petro kabla hajamuombea kiwete alimwambia tutazame sisi (Matendo ya mitume 3:4,6-9)
NB: Yesu Yuko ndani yako unapomtazama mtu anayesumbuliwa na nguvu za Giza kuna vitu vitakuwa vinaingia ndani yake kushughulikia nguvu hizo za Giza.
6.ZINGATIA UFUNUO UNAOPEWA NA ROHO MTAKATIFU WAKATI WA MAOMBEZI
-Kuna wakati Mungu huwapa watu mafunuo ya namna mbalimbali wakati wa maombezi.
(Marko 8:23-26)
Yesu alimtemea mate kipofu Kisha akamuwekea mikono.
(2 Wafalme 5:9-10)
Naamani aliambiwa akaoge kwenye mto Yordani mara Saba atapona, alipozingatia ufunuo huo alipona.
(Yohana 9:1-7)
Yesu alitema mate akatengeneza tope akampaka kipofu machoni Kisha akamwambia aende kunawa kwenye birika ya Siloamu, yule kipofu alipofanya alichoelekezwa alipona kabisa.
NB: Ufunuo ambao Roho Mtakatifu anakupa wakati unamuombea mtu ni wa muhimu sana katika kumsaidia unayemuombea.
7.MUOMBE MUNGU AKUREJESHEE NGUVU ZILIZOKUTOKA PIA AKUONGEZEE NGUVU
(Waefeso 3:20)
– Ukimuombea mtu Pepo wakamtoka, magonjwa yakapona nakadhalika ni vema ufahamu kuwa Kuna nguvu huwa zinatoka ili kusababisha mambo hayo yatokee.
(Luka 8:46-48)
Yesu alipoguswa na mwanamke aliyetokwa damu, yule mwanamke alipona kwa kuwa Kuna nguvu zilimtoka Yesu zikaponya tatizo la yule mwanamke.
NB: Usiishie kufurahia watu wanapona unapowaombea, popo wanatoka nakadhalika, baada ya hayo kutokea hakikisha unaomba nguvu mpya kutoka kwa Mungu.
8. UIMBAJI NA MUZIKI
Uimbaji na Muziki ni muhimu wakati wa maombezi, kama Kuna uwezekano wa kuimba ni muhimu kuimba kabla ya kumuombea mtu kwa kuwa uimbaji na Muziki ni moja ya funguo ya mambo mbalimbali ikiwemo nguvu za Mungu.
(2 Wafalme 3:11-20)
Mpiga kinanda alipopiga ndipo unabii ukaachiwa kutoka kwa Mungu.
NB: "Nimeona wakati wa kuimba Pepo wakiwatoka watu hata kabla hawajaombewa" Faraja Gasto.
Mungu akubariki kwa haya machache.
0 Maoni