KUTIANA MOYO


 ✍️Faraja Gasto


Utangulizi

Katika safari yetu ya kwenda mbinguni tunakutana na mambo mengi sana ya kuumiza na yanayovunja moyo.


Kutokana na kutokutiana moyo, wengi wamerudi nyuma, hawana nguvu za kuendelea na safari, wamebaki katika hali ya kuchoka.


 BAADHI YA SABABU KWA NINI TUTIANE MOYO?

✓Kila mwanadamu hupatwa na majaribu mbalimbali. (1 Wakorintho 10:13)


✓Kila mwanadamu huwa kuna wakati anajisikia kuchoka.

–Wengine huchoka kumwomba Mungu, wengine huchoka kwenda ibadani, wengine huchoka kumtumikia Mungu nakadhalika.



✓Kila mwanadamu huwa kuna wakati anakata tamaa kabisa kutokana na sababu mbalimbali.


—Neno la Mungu linasema Nabii Eliya alipopata taarifa kuwa Yezebeli ameapa kumuua, Nabii Eliya alikimbia akiwa amekata tamaa kabisa na akamuomba Mungu amuondoe duniani (1 Wafalme 19:1-4)


Kwa kuwa hapakuwa na mtu wa kumtia moyo, Nabii Elisha aliona hakuna umuhimu wa kuendelea na huduma, hakuna umuhimu wa kuendelea kuishi.


 UMUHIMU WA KUTIANA MOYO

✓Kutia moyo huleta nguvu mpya, matumaini mapya na mtazamo mpya ndani ya mtu.


(Isaya 41:6-7)

Neno la Mungu linasema wenzetu walitambua Kila kinachofanywa na mwingine ni Cha tahamani, Kila mtu kwa nafasi yake ni wa thamani kwa hiyo walitiana moyo.


Kadiri walivyozidi kutiana moyo ndivyo walivyozidi kuhamasika kuendelea na kazi walizokuwa wakifanya.


(Ezra 10:4)

Biblia inasema Ezra aliambiwa "inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende"


Ezra alivyotiwa moyo alipata nguvu zaidi za kuendelea na majukumu yaliyompasa kuyatekeleza.


✓Kutia moyo humfanya mtu aone changamoto au majaribu anayopitia ni ya kawaida.


Mtume Paulo alipokuwa akiwatia moyo Wakorintho kutegemeana na majaribu waliyoyapitia aliwaambia kuwa wanapaswa kufahamu kuwa jaribu lililowapata wao sio jipya bali limewahi kuwapata wengine kwa kuwa ni jambo la kawaida mwanadamu kupatwa na majaribu mbalimbali (1 Wakorintho 10:13).


BAADHI YA MBINU ZA KUTIANA MOYO 

✓Kuwatuliza watu moyo (kuwafariji)

(Isaya 40:1)

—Moyo uliovunjika humfanya mtu kukosa utulivu lakini anapopata mtu wa kumtia moyo, mtu huanza kupata utulivu hatimaye huendelea na safari, huendelea na utumishi nakadhalika.


✓Kuambiana maneno mazuri.

(Mithali 15:4)

Ulimi unaotoa maneno mazuri hutia moyo lakini ulimi unaotoa maneno mabaya huvunja moyo.


✓Kuwapongeza wanaofanya vizuri.

(Isaya 41:6-7)

Hawa watu walipongezana, kupongezana huko kuliwafanya wakatiana moyo wa kufanya vizuri zaidi.


Mtu akifanya vizuri anapaswa kupongezwa, kumpongeza kwa maneno pia kupongezana Kwa kupeana zawadi.


✓Kufundishana neno la Mungu au kusemezana neno la Mungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni