✍️Faraja Gasto
Hakuna tafsiri ya kidunia kuhusu maendeleo (there is no universal definition of development) hivyo basi maendeleo yamekuwa yakitafsiriwa Kwa namna tofautitofauti.
Kuna tafsiri inasema, maendeleo ni kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine iliyo Bora zaidi.
BAADHI YA KANUNI ZA MAENDELEO (PRINCIPLES OF DEVELOPMENT)
✓KUAMBATANA
Kanuni ya kuambatana inasema hivi "hakuna aliyewahi kuendelea mwenyewe bila mchango wa watu wengine kwa hiyo ili uendelee unahitaji watu wa kuambatana nao"
Mwalimu J.K Nyerere aliwahi kusema ili tuendelee tunahitaji mambo manne; watu, uongozi Bora, siasa safi na ardhi.
Mtu mmoja alisema "ukitaka kwenda haraka nenda peke Yako ila ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako"
Uambatane na nani
*Ambatana na watu mnaofanana kimaono, kikazi nakadhalika.
*Ambatana na watu wenye mchango katika unachofanya, unachopanga kufanya.
*Ambatana na watu mnaopatana.
✓JIFUNZE KWA WENGINE
Kuna tofauti ya kuiga Kwa wengine na kujifunza Kwa wengine, kujifunza Kwa wengine ni kuchukua mambo muhimu yaliyowafikisha hapo walipo.
Aina yoyote ya maisha unayotaka Kuna watu tayari wanaishi maisha hayo, kanuni rahisi ya kuishi maisha hayo ni kujifunza kutoka kwao.
✓KUWEKA MALENGO
Kama haujui unataka kwenda wapi na kwa nini uende hapo si rahisi kupiga hatua, Si rahisi kupata nguvu au hamasa ya kwenda.
Kuweka malengo itakusaidia kuchukua hatua, itakupa hamasa ya kufanya juu chini ili ufike pale unapotaka ufike.
✓MATUMIZI YA FEDHA
Fedha zina nafasi yake katika maendeleo, ukizitumia ipasavyo utapiga hatua ila ukitumia fedha vibaya utabaki vilevile.
Matumizi sahihi ya fedha ni yapi?
*Kumtolea Mungu
*Kuwekeza
*Kula Kwa utaratibu (usile chochote maadamu una pesa, jiwekee utaratibu)
*Vaa kwa utaratibu (usinunue nguo Kwa kuwa mwingine amenunua)
*Jenga nyumba n.k
Matumizi mabaya ni yapi?
*Anasa, kutumia fedha Kwa ajili ya vitu visivyo vya lazima
*Kutumia fedha kiholela (mtu akiomba tu umeshampa, mtu akikusifia tu umeshampa, kutaka uonekane unazo fedha.
Mambo ya kukusaidia ili uwe na matumizi mazuri ya fedha
*Soma neno la Mungu
*Epuka matumizi yasiyo ya lazima
*Tengeneza bajeti yako binafsi, familia nakadhalika.
✓UWE TAYARI KULIPA GHARAMA
Hakuna chochote kizuri kimewahi kutokea kwenye Dunia hii bila gharama fulani, lazima uwe tayari kulipa gharama za aina mbalimbali ili upige hatua.
✓BIDII
Maendeleo hayaji kwa watu wavivu, lazima uwe mtu mwenye bidii katika mambo Yako, kama ni kazi fanya Kwa bidii, kama unasoma soma Kwa bidii.
0 Maoni