KUMPENDEZA MUNGU


 ✍️Faraja Gasto

Mungu anataka tumpendeze yeye yaani tutende yale anayotaka tuyatende.

Kumpendeza Mungu kunaanza na kujua mambo ambayo Mungu anayataka (yale anayoyapenda), kujua maelekezo yake kuhusu mambo mbalimbali.

Ndio maana Biblia inasema "pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu" (Waebrania 11:6)

Ili tuwe na imani lazima tuwe na neno la Mungu mioyoni mwetu kwa kuwa imani huja kwa kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17)

Kwa hiyo hauwezi kumpendeza Mungu kama huna neno la Mungu moyoni mwako, Mfalme Daudi alitambua kuwa haiwezekani kumpendeza Mungu kama hauna neno lake moyoni ndio maana Mfalme Daudi alisema

"moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisije nikakutenda dhambi" (Zaburi 119:11)


Chapisha Maoni

0 Maoni