TANGULIZI
Watu wengi wamemwamini Yesu lakini sio wote wanaomjua waliyemwamini, wengi hawamjui Yesu kwa undani, kwa marefu na mapana.
Yesu alipokuwa na wanafunzi wake chomboni ghafla dhoruba ilitokea, wanafunzi wakatumia utaalamu wao wa kuijua bahari ili kukabiliana na ile hali lakini hali haikuwa shwari, wakamwendea Yesu wakamuamsha Yesu akakemea Pepo na na Bahari ghafla kukawa shwari kuu, wanafunzi wa Yesu walisemezana "huyu ni mtu wa namna gani hata Pepo na Bahari zinamtii"(Mathayo 8:23-27)
Kauli hiyo inathibitisha kuwa walikuwa na Yesu wamemwamini lakini walikuwa hawajajua Yesu ni wa namna gani.
Watu wengi wanamwamini Yesu ni Bwana na mwokozi lakini hawamjui ni wa namna gani.
Mtume Paulo alisema "ninamjua niliyemwamini" (2 Timotheo 1:12)
Mtume Paulo aliwaombea Waefeso wapewe roho ya hekima na ya ufunuo ili wamjue Mungu (Waefeso 1:15-17)
YESU NI NANI?
Yesu ni Mungu mwana aliyeumba Dunia na vyote vilivyomo (Yohana 1:1-3).
Yesu alipozikemea pepo na Bahari zilimtii kwa kuwa zinajua yeye ndiye muumbaji (Mathayo 8:27)
Kwa hiyo Yesu ni Mungu halisi hakuna gumu asiloliweza.
FAIDA CHACHE ZA KUMJUA ULIYEMWAMINI
✓Hofu itakuwa mbali na wewe.
Shadraka, Meshaki na Abednego hawakuogopa tanuru ya moto kwa kuwa walikuwa wanamjua Mungu waliyemwamini anaweza kuwaokoa na moto maana yeye ndiye aliyeumba moto (Danieli 3:16)
Daudi hakumuogopa Goliathi kwa kuwa alikuwa anamjua Mungu aliyemuwezesha kuua Simba na dubu atamuwezesha kumuua Goliathi (1 Samweli 17:32-37)
Daudi hakuogopa mambo mbalimbali yaliyokuwa tishio kwa kuwa alikuwa anamjua Mungu aliyemwamini anaweza kumuokoa na hali za hatari (Zaburi 23:1-4)
NB: Ukimjua Mungu hautaogopa hatari mbalimbali kwa kuwa Mungu uliyemwamini ni bingwa wa kuokoa watu wake.
✓Ni rahisi kupata ufumbuzi au suluhisho la tatizo au matatizo.
Watu wengi hujikuta wakikosa suluhisho au ufumbuzi wa tatizo au matatizo Kwa sababu hawamjui Mungu.
Goliathi alikuwa tatizo kwa waisraeli, Daudi alikuwa suluhisho la tatizo la waisraeli kwa kuwa alikuwa anamjua Mungu.
Daudi kumjua Mungu anaweza kumuokoa na mkono wa Goliathi, Daudi alilikabili lile tatizo na likapata suluhisho (1 Samweli 17:32-37)
UTAMJUAJE ULIYEMWAMINI?
✓Soma sana neno la Mungu (Biblia)
Ukisoma neno la Mungu utaona jinsi Mungu alivyofanya mambo ya kushangaza, utajua uwezo wa Mungu utazidi kuimarika kiimani.
✓Muombe Mungu ajifunue kwako umjue.
Yamkini umekuwa ukisikia tu habari za Mungu, matendo yake makuu nakadhalika lakini matendo makuu ya Mungu hayajawahi kuwa halisi kwako, muombe Mungu ajifunue kwako ili umjue.
0 Maoni