KUMPA MUNGU NAFASI YA KUMSIKILIZA


✍️Faraja Gasto

UTANGULIZI

Watu wengi wanapenda sana kusikilizwa na Mungu lakini ni vema Kila mtu afahamu kuwa hata Mungu anapenda kupewa nafasi ya kusikilizwa (Zaburi 81:13-16)


KWA NINI UMSIKILIZE MUNGU?

1.Mtu aliumbwa ili aishi kwa maelekezo ya neno la Mungu (Mathayo 4:4)


2.Mungu anapenda kusikilizwa kama jinsi ambavyo unapenda kusikilizwa na yeye (Zaburi 81:13-16)


MBINU RAHISI ZA KUMSIKILIZA MUNGU

1.Soma neno la Mungu au jifunze sana neno la Mungu.


Mungu huongea na watu kupitia neno lake (Zaburi 107:20) unapolisoma neno la Mungu au kujifunza neno la Mungu utaanza kumsikia Mungu aliongea na wewe.


2.Waendee watumishi wa Mungu.

–Zamani watu walikuwa wakiwaendea watumishi wa Mungu ili kusikia Mungu anasema nini kuhusu wao (Yeremia 42:1-22) (2 Wafalme 3:11-20)


— Hata sasa Mungu anazungumza na watu kupitia watumishi wake waliopo duniani, jifunze kuwaendea watumishi wa Mungu zungumza nao.


3.Jifunze kuwa na muda wa kutulia ili kumpa Mungu nafasi ya kuongea na wewe ikiwa analo jambo la kukuambia.


(2 Mambo ya Nyakati 20:5-19)

Hawa watu walimuomba Mungu na wakampa Mungu nafasi ya kumsikiliza.


(Habakuki 2:1-3)

Nabii Habakuki alimuomba Mungu Kisha akampa Mungu nafasi ya kumsikiliza, Mungu alipopewa nafasi ya kuongea aliongea.


HITIMISHO

Kama jinsi ambavyo wewe unavyopenda kusikilizwa na Mungu, Mungu naye anapenda umsikilize, mpe Mungu nafasi ya kumsikiliza.

Chapisha Maoni

0 Maoni