✍️ Faraja Gasto
(Esta 1:10-20)
Huu ni ujumbe maalumu kwa Kila mwanamke aliyeolewa, natoa wito Kila mwanamke asome ujumbe huu maana Kuna jambo la kumsaidia.
Kumekuwepo na kuongezeka Kwa malalamiko mengi wanawake wengi wakilalamika kuwa waume zao wanatoka nje ya ndoa wengine wameamua kuacha miji yao na kwenda kuoa wanawake wengine.
Nataka Kila mwanamke aelewe siri hii itamsaidia sana katika ndoa yake.
Ukisoma Kitabu Cha Esta sura ya kwanza mstari wa kumi mpaka mstari wa ishirini utakutana na habari ya Mfalme Ahasuero, wakati fulani Mfalme Ahasuero alifanya sherehe katika ufalme wake wakati sherehe ikiendelea alituma watu wamuite malkia Vashti (mke wa Mfalme) Mfalme alitaka awaonyeshe watu jinsi mke wake alivyo mzuri lakini Vashti alipoitwa alikataa kuja.
Kitendo Cha kukataa wito wa Mfalme kilitafsiriwa kama ni dharau, kutokana na dharau hiyo washauri wa Mfalme waliitwa waseme neno, ndipo ukatoka ushauri kuwa NAFASI YA VASHTI APEWE MTU MWINGINE.
DHARAU ndio ilisababisha Vashti akatolewa kwenye nafasi ya umalkia na nafasi yake akaichukua Esta.
MWANAMKE UNAPASWA KUFAHAMU kuwa tabia ya kumdharau mume wako na kutonyenyekea kwake itakufanya umkose huyo mume, wanawake wengine wameachwa au wametelekezwa Kwa sababu ya dharau zao, mwanamke epuka dharau nyenyekea kwa mumeo.
Wengine nafasi zao zimechukuliwa na wasaidizi wa kazi (house girls), wengine nafasi zao zimechukuliwa na makahaba, wengine nafasi zao zimechukuliwa na marafiki zao, ndugu zao nakadhalika. Ni vema mwanamke ufahamu kuwa mwanamume ni kichwa hebu nyenyekea kwake.
NB: Si Kila mwanamume anayetoka nje ya ndoa au anayekimbia mji na kuoa mwanamke mwingine ni kwa sababu ya tamaa, wengine wamekimbia dharau za wake zao wakaenda kutafuta wanawake wengine watakaowanyenyekea na kuwaheshimu.
Pia simaanishi mwanamke anapaswa kudharauliwa pia sihamasishi wanaume kuwaacha wake zao Kwa kuwa wana dharau ila nimetumia kisa Cha Mfalme Ahasuero kuwafundisha wanawake kuwanyenyekea waume zao na kuwaheshimu kwa sababu nyenzo mojawapo ya kulinda ndoa Yako ni unyenyekevu.
0 Maoni