HAPATAKUWA NA MTU ATAKAYEWEZA KUSIMAMA MBELE YAKO SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO


✍️Faraja Gasto

(Yoshua 1:5)

Mungu alimwambia Yoshua mambo mengi, jambo mojawapo ambalo Yoshua aliambiwa ni "hapatakuwa na mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha Yako"

Maana yake

1.Hapatakuwa na mtu atakayeweza kumshinda yaani ni sawa na kusema watashindana nawe lakini hawatakushinda.

2.Hakuna mtu atakayekuzuia kufika kule ninakotaka ufike.

3.Wewe ndiwe utakayekuwa mbele kwa kuwa hakuna atakayesimama mbele yako siku zote za maisha Yako.

Nini hutokea mtu anapokuwa mbele yako 

1.Kile ambacho unatakiwa kupata hautapa, atakipata yeye 

(Yohana 5:7) kiwete aliyekutwa na Yesu birikani alisema ninapotaka kwenda mbele Kuna mwingine hutokea na kwenda mbele akapona yeye ndio maana Mimi nipo tu sijapona.

2. Aliye mbele ndiye anayeamua mambo mbalimbali (nini upate, nini ukose, nini uone nakadhalika)

(Mwanzo 45:4-5) Yusufu aliwaambia ndugu zake kuwa Mungu alimpeleka mbele yao ili kuhifadhi maisha ya watu, walipata maisha mazuri kwa kuwa aliyekuwa mbele ni ndugu yao.

(Luka 19:1-3) Waliokuwa mbele ya Zakayo walisababisha Zakayo asimuone Yesu, kilichosababisha Zakayo akamuona Yesu ni kwa sababu alitangulia mbele akapanda juu ya mkuyu (Luka 19:4)

3.Aliyetangulia mbele ndiye huwa anafahamu kabla ya wengine, ataona kabla ya wengine pia atapata kabla ya wengine.

(Yohana 5:7) Aliyetangulia mbele alipata uponyaji.

(Hesabu 13:25-28) Wapelelezi waliifahamu nchi ya Kanaani kabla wengine hawajaifahamu, waliona nchi kabla ya wengine.

MAOMBI

  1. Omba Mungu akupeleke mbele.

2.Omba Mungu apeleke mbele watu sahihi.

Chapisha Maoni

0 Maoni