✍️Faraja Gasto
UTANGULIZI
Neno "mtoto" hutafsiriwa kwa namna mbalimbali kutegemeana na muktadha husika, Kwa mfano kwa mujibu wa muktadha wa sheria mbalimbali zinatafsiri mtoto ni mtu yeyote aliye na umri chini ya miaka 18.
Katika muktadha wa kiutamaduni, mtoto ni mtu yeyote aliyezaliwa (mtu yeyote mwenye wazazi) bila kujali umri.
Pia katika muktadha wa dini, neno "mtoto" hutafsiriwa kwa namna mbalimbali kutegemeana na dini husika.
Ninapofundisha somo hili nataka tumtazame mtoto kama mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18, mtu yeyote aliye katika kipindi cha ujana na mtu yeyote ambaye bado analelewa na wazazi wake.
SOMO LENYEWE
Unapowatazama watoto unapaswa kuwatazama katika mtazamo mpana ikiwemo kuwatazama watoto kama wazazi wajao.
Ukishafahamu kuwa watoto ni wazazi wajao anza kuwajenga kama wazazi wajao, baadhi ya mambo unayopaswa kuwafundisha ni;-
1. Wafundishe watoto wamjue Mungu wa mbinguni.
2. Wafundishe watoto nidhamu katika masuala mbalimbali mahusiano, fedha nakadhalika.
3. Wafundishe watoto kufanya kazi za nyumbani na kazi zingine halali bila kuwaathiri.
4. Wafundishe watoto kuishi vizuri na watu.
5. Wafundishe watoto kupambanua mema na mabaya.
6. Wajengee watoto uwezo wa kujieleza.
7. Wafundishe watoto uwajibikaji, wajue wajibu wao katika maisha yao, wajibu wao katika maisha ya wengine nakadhalika.
NB: Ni muhimu kuzingatia rika la mtoto katika kumjenga mtoto kupitia mafundisho fulani.
0 Maoni