✍️ Faraja Gasto
Siku moja nikiwa kwenye gari aliingia kijana mmoja akasimama mbele yangu Kisha gari likaanza safari ghafla nikasikia sauti moyoni mwangu ikiniambia "Kuna viwango vya upendo ambavyo watu wengi hawajavifikia" kiwango kimojawapo cha upendo ambacho watu wengi hawajakifikia ni KIWANGO CHA KUWAPENDA WENGINE KAMA TUNAVYOJIPENDA WENYEWE (Wafilipi 2:3c)(Marko 12:31)
Ile sauti ikaniambia kama ningekuwa nimefika kwenye kiwango hicho cha upendo ningemuachia kiti yule kijana aliyesimama halafu mimi nikasimama, hiyo ndio maana halisi ya kumpenda jirani yako kama nafsi yako au kama unavyojipenda mwenyewe.
NB: Mpende jirani yako kama nafsi yako.
0 Maoni