NEEMA


  ✍️ Faraja Gasto

Neno neema (grace) limekuwa linatafsiriwa kwa namna mbalimbali, wengine wanasema neema ni kibali, upendeleo, majaliwa nakadhalika.

Neema ni nini?

Biblia inataka tufahamu kuwa neema

Neema ni uwezesho unaotokana na utendaji kazi wa Roho Mtakatifu.

Neema ni uwezesho unaokufanya kuweza au kufanya mambo ambayo kwa nguvu zako usingeweza, kwa fedha zako usingeweza, kwa ajili zako usingeweza, kwa jitihada zako usingeweza.

Kwa mfano, bila neema ya Mungu hakuna anayeweza kuacha dhambi, neema ndio inaweza kumsaidia mtu kuacha dhambi. 

Nataka nikufundishe sababu chache kwa nini Yesu alileta Neema (Yohana 1:17)

Wokovu ni tunda la neema 

Wokovu ni msamaha wa dhambi, msamaha wa dhambi tunaupata kupitia neema ya Mungu iliyokuja kupitia Yesu Kristo.

Neema inaweza kumbadilisha mtu.

(1 Wakorintho 15:10) neema ndio ilimfanya Sauli kubadilika kisaikolojia (hisia, mtazamo, akili nakadhalika) ndio maana anashuhudia kwamba kilichombadilisha ni neema ya Mungu.

AINA ZA NEEMA 

Kuna makundi makuu mawili ya neema

Neema kuu (general grace)

Hii ndio neema inayoleta wokovu (msamaha wa dhambi), soma (Yohana 1:17) (Tito 2:10-11) (Waefeso 2:8-9)

Neema maalumu (special grace)

Neema maalumu zipo za aina mbalimbali ndio maana kila mtumishi wa Mungu ndani ya Kristo Yesu kuna neema anayo au anazo.

Kwa mfano Mariamu mama yake Yesu alipewa neema maalumu ya kumbeba Yesu tumboni na kumzaa (Luka 1:28) hii inaitwa neema ya kubeba na kuzaa ambacho Mungu anataka kizaliwe,  Barnaba alikuwa na neema ya kufariji (Matendo ya mitume 4:36), makanisa ya Makedonia yalipewa neema ya ukarimu (2 Wakorintho 8:1-2), Mtume Paulo alipewa neema ya kuhubiri injili kwa mataifa (Wagalatia 2:9) neema aliyopewa Mtume Paulo ndio ilimuwezesha kufanya kazi kubwa sana kuliko hata mitume waliokuwa pamoja na Yesu. Hizo ni baadhi ya neema maalumu ambazo Mungu huwapa watu.

MAMBO MACHACHE YA KUKUSAIDIA KUPATA NEEMA MAAALUMU

Unyenyekevu

Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu (1 Petro 5:5) ni muhimu sana ujifunze kunyenyekea kwa Mungu na kwa watumishi wake maana wana neema ambazo wanaweza kuziachilia juu yako.

Omba Mungu akupe neema.

Yesu alisema ombeni lolote kwa jina langu nanyi mtapewa, kwa hiyo unaweza kuomba neema fulani Kwa Mungu (Yohana 16:23)

NB: 

Neema ni ya muhimu katika kila eneo la maisha yako, unahitaji neema katika kuhubiri, kufundisha, kuomba, kuimba, kufanya siasa, kufanya biashara nakadhalika. Neema ya Mungu inaweza kukufanya ukatenda mambo ambayo usingeweza kwa akili zako, nguvu zako, fedha zako nakadhalika.

Nakuhimiza kusoma Biblia ili ujifunze mambo mengi kuhusu neema ili uone ilivyo ya muhimu sana katika kila eneo la maisha yako.

3. Ni muhimu sana kutambua na kuheshimu neema zilizo juu watu zisaidie mambo mbalimbali katika mwili wa Yesu Kristo ili kuwepo na urahisi wa kufanikisha mambo mbalimbali. Kwa mfano mitume Petro, Yohana na Yakobo walipojua neema iliyoko juu ya Mtume Paulo alimpa mkono wa shirika wakagawana majukumu (Wagalatia 2:8-9) kazi ya kueneza injili ikafanyika Kwa Kasi.

Chapisha Maoni

0 Maoni