KUTAFUTA SULUHU YA MATATIZO YANAYOWAKABILI UNAOWAONGOZA


✍️ Faraja Gasto

Kama wewe ni kiongozi (wa familia, taasisi, siasa nakadhalika) Wajibu mmojawapo wa kiongozi yeyote ni kutafuta suluhu ya matatizo yanayowakabili unaowaongoza, mtu yeyote anayejikita kutafuta suluhu la matatizo ya watu huyo ndio anafaa kuitwa kiongozi.

Mifano ya viongozi na namna walivyotafuta suluhu ya matatizo mbalimbali 

MFANO WA 1: MFALME DAUDI DHIDI YA TATIZO LA NJAA

(2 Samweli 21:1-10)

Kulikuwa na njaa nzito wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, Mfalme kama kiongozi alitafuta suluhu la tatizo lile kwa njia ya kumuomba Mungu, Mungu akampa maelekezo ya kutatua tatizo lile.

MFANO WA 2: IBRAHIMU DHIDI YA UGOMVI WA WACHUNGAJI 

(Mwanzo 13:7-1)

Kutokana na utajiri wa Ibrahimu na Lutu kulitokea ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Ibrahimu na wachunga mifugo wa Lutu.

Ibrahimu kama kiongozi wa familia aliamua watengane yeye na Lutu, yeye akae kwingine na Lutu akakae kwingine ili kuepuka migogoro.

MFANO WA 3: MUSA DHIDI YA TATIZO LA MAJI

(Kutoka 17:1-6)

Wana wa Israeli katika kusafiri kwao walifika mahali hapakuwa na maji, kukawa na tatizo la maji mpaka watu wakaanza kunung'unika, Musa alimlilia Mungu akampa maelekezo ya namna ya kutatua tatizo hilo.

MFANO WA 4: MITUME DHIDI YA MANUNG'UNIKO YA WAYAHUDI WA KIYUNANI

(Matendo ya mitume 6:1-6)

Kulitokea manung'uniko kutokana na kusahauliwa kwa baadhi ya wajane katika mgao wa Kila siku.

Mitume waliitisha kikao cha kanisa wakachaguliwa watu waliosimamia jambo lile ili mambo yaende vizuri kusiwepo manung'uniko.

HITIMISHO

Kila kiongozi anapswa kufahamu kuwa ana wajibu wa kutafuta suluhu ya matatizo yanayowakabili watu anaowaongoza.

Chapisha Maoni

0 Maoni