NAFASI YA MWANAMKE KATIKA HESHIMA YA MWANAMUME


✍️Faraja Gasto

Mwanamke ni kama mlinda mlango (goal keeper) mwanamume ni kama mshambuliaji. Timu yoyote hata kama ina wachezaji wazuri ikiwa ina mlinda mlango asiye na uwezo wa kulinda vizuri lazima timu hiyo itakuwa inafungwa au inashindwa kwenye mashindano.

Mlinda mlango ndiye huamua kuhusu heshima ya timu, akilinda vema mlango timu yake haitashindwa, ndivyo alivyo mwanamke ni kama mlinda mlango anaweza kuzuia aibu, fedhedha nakadhalika.

 (Waefeso 5:33b)

Biblia inaposema mke asikose kumstahi mumewe maana yake ni kwamba mke anao wajibu wa kulinda heshima ya mume wake.

Kama Kuna mambo unaona yatavuruga heshima ya mume wako una wajibu wa kutafuta njia ya kuhakikisha unalinda heshima ya mumeo, hili linakwenda sambamba na kutomdhalilisha mumeo, kutotangaza udhaifu wake nakadhalika.

(1 Samweli 25:2-35)

Daudi alikusudia kumuangamiza Nabali, familia yake na Mali zake lakini mke wa Nabali alijinyenyekeza kwa Daudi hata Daudi akaahirisha mpango alipokuwa nao. Busara ya Abigaili ililinda heshima ya mumewe.

HITIMISHO

Mwanamke una wajibu wa kulinda heshima ya mume wako, wewe unaweza kusababisha mume wako aheshimiwe au adharauliwe, anza kumuheshimu mume wako pia acha watu wafahamu kuwa unamuheshimu mume wako.

Chapisha Maoni

0 Maoni