✍️Faraja Gasto
Yamkini umefika hatua umejikuta njia panda kimaamuzi haujui uamue kipi, nataka nikuambie kuwa Mungu ana maelekezo ya kukutoa hapo njia panda.
Nataka ujifunze kupitia mifano hii ya watu waliokuwa njia panda kimaamuzi na namna Mungu alivyowasaidia.
MFANO WA 1: MFALME YEHOSHAFATI
(2 Mambo ya Nyakati 20:1-18)
Majeshi kadhaa yalijipanga ili kuhakikisha Mfalme Yehoshafati na watu wake wanashambuliwa, Mfalme Yehoshafati akawa kwenye wakati mgumu kimaamuzi maana hakujua afanye nini ili kukabiliana na majeshi yale, ikabidi atangaze mbiu ya watu kufunga ili kumtafuta Mungu.
Walipomtafuta Mungu aliwapa maelekezo yaliyopelekea wakafanya maamuzi mazuri yaliyopelekea ushindi.
MFANO WA 2: WANA WA ISRAELI
(Kutoka 14:10-16)
Ilifika hatua wana wa Israeli wakawa njia panda kimaamuzi hawajui wafanye nini Kwa kuwa nyuma waliona Jeshi la Mfalme Farao linakuja halafu mbele yao Kuna bahari ya Shamu.
Musa akamlilia Mungu, Mungu akampa maelekezo ya kufanya ili kuigawanya bahari wana wa Israeli wapite.
HITIMISHO
Mungu huwapa watu maelekezo kwa njia mbalimbali kama vile ndoto, maono, neno lake unapolisoma, ushauri, mawazo yake kuletwa ndani yako nakadhalika.
Usiendelee kubaki njia panda, mwambie Mungu akupe maelekezo yake ili yakusaidie kufanya maamuzi sahihi yatakayosababisha matokeo chanya.
0 Maoni