✍️Faraja Gasto
Kila mtu anatamani kuinuliwa na Mungu yaani awe mtu wa kuheshimiwa katika jamii, apandishwe vyeo, awe mtu mwenye uchumi mzuri nakadhalika.
Unapaswa kufahamu kuwa katika kuelekea kwenye kuinuliwa utakutana na mambo mbalimbali ikiwemo yanayovunja moyo, kudhalilishwa, vitisho, kuchekwa nakadhalika, usiogope kwa kuwa mambo hayo hayana budi kutokea maadamu unapita kwenye njia ya kuelekea kuinuliwa lazima ukutane nayo.
Nataka ujifunze kupitia mifano hii michache ya watu walioinuliwa na Mungu uone mambo waliyokutana nayo njiani walipokuwa wakielekea kwenye kuinuliwa;-
MFANO WA 1: BWANA YESU KRISTO
(Mathayo 28:18)
Baada ya Yesu kufufuka alisema "mamlaka yote ya mbinguni na duniani amepewa"
Kabla hajainuliwa kwenye kiwango hicho alitemewa mate, alidhihakiwa, alichomwa mkuki nakadhalika.
Baada ya hayo yote AKAINULIWA SANA HATA AMEKUWA BWANA WA MABWANA TENA MFALME WA WAFALME.
MFANO WA 2: YUSUFU MTOTO WA YAKOBO
(Mwanzo 41:41-46)
Mungu alimuinua Yusufu akawa na cheo kikubwa katika serikali ya nchini Misri lakini kabla hajainuliwa alichukiwa na ndugu zake, ndugu zake walitaka kumuua, walimuuza kwa wafanya biashara, wafanya biashara nao wakamuuza kwa Potifa, alipokuwa Kwa Potifa akasingiziwa amembaka mkewe Potifa, Yusufu akafungwa jela hatimaye Mungu alimuinua kutokea jela.
HITIMISHO
Nimekutazamisha mifano hiyo ili ufahamu kuwa katika kuelekea kwenye kuinuliwa na Mungu utakutana na mambo mbalimbali mepesi na magumu, USIOGOPE ENDELEA KULINDA IMANI YAKO NA KUSONGA MBELE BILA KUJALI UNAYOKUTANA NAYO NJIANI.
0 Maoni