UKWELI KUHUSU MATUKIO YA UKATILI NA SULUHISHO LAKE


✍️ Faraja Gasto

Imekuwa si ajabu kusikia au kuona watu wakifanyiwa ukatili wa aina mbalimbali kutegemeana na sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitajwa.

Vyanzo ambavyo vimekuwa vikielezwa kama visababishi vya ukatili ni wivu wa kimapenzi, hasira kali, imani za kishirikina nakadhalika.

JAMBO MOJAWAPO TUNALOFAHAMISHWA NA BIBLIA KUWA NI CHANZO CHA   UKATILI

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Ukatili ni matokeo ya giza kutawala au ukatili ni matokeo ya ufalme wa giza kutawala.

Zaburi 74:20

Ulitafakari agano; Maana mahali PENYE GIZA katika nchi PAMEJAA MAKAO YA UKATILI.

Kwa hiyo ukatili ni matokeo ya utendaji kazi wa ufalme wa giza.

Usidhani watu hawafahamu kama ni makosa kumfanyia mtu ukatili, ingawa wanafahamu kwamba kutenda ukatili ni kosa la jinai lakini bado wanafanya ukatili, HILI LINATOSHA KUKUJULISHA KUWA CHANZO CHA UKATILI NI UFALME WA GIZA.

NINI KIFANYIKE KUKABILIANA NA VITENDO VYA UKATILI

1. Kuhubiri injili.

Yohana 1:5

Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

Hapo juu tumeona kuwa ukatili ni matokeo ya utendaji kazi wa ufalme wa giza Kwa hiyo ili tukabiliane na ukatili ni muhimu watu wamwamini Yesu (Nuru).

Yesu ni Nuru, watu wakimwamini hawatafanyiana vitendo vya ukatili kwa kuwa Nuru ikiingia giza linatoweka na matokeo ya giza yanakoma.

2. Kuhakikisha watu wanatawaliwa na Roho Mtakatifu.

Wagalatia 5:22-23

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi.

Ukatili ni tendo lisilotokana na upendo pia ni tendo lisilo la utu wema, kama ni tendo lisilo la upendo na lisilo la utu wema basi ni tendo linalotokana na roho chafu.

Mtu akiwa na Roho Mtakatifu atakuwa na utu wema, utu wema ukitawala basi hawezi kutenda ukatili.

NB: Sheria hazitoshi kukomesha ukatili ndio maana sheria zipo lakini ukatili bado unakithiri, WATU WANAMUHITAJI YESU KRISTO, JAMII INAMUHITAJI YESU KRISTO NDIYE SULUHISHO PEKEE LA VITENDO VYA UKATILI.

Chapisha Maoni

0 Maoni