a). Akili ni uwezo wa kuelewa.
b). Akili ni ufahamu.
BAADHI YA USHAHIDI WA BIBLIA UNAOONYESHA NENO LA MUNGU NI CHANZO CHA AKILI
USHAHIDI WA 1
(Mwanzo 41:33,39)
Mfalme Farao alishauriwa atafute mtu mwenye akili na hekima, haina maana kwamba pale Misri hawakuwepo wenye akili na hekima ila KUNA AINA YA AKILI NA HEKIMA ILIYOKUWA INAHITAJIKA KWA WAKATI HUO ndio maana Mfalme Farao aligundua kuwa hakuna mtu mwenye hiyo akili na hekima isipokuwa Yusufu peke yake.
Yusufu alikuwa na aina ile ya akili Kwa kuwa alikuwa na neno la Mungu moyoni mwake, lile neno la Mungu ndilo lilimfanya akaonekana ana akili.
USHAHIDI WA 2
(Mathayo 7:24-25)
Yesu alitoa mfano unaoonesha neno la Mungu kama chanzo cha akili, Yesu alisema "Basi kila asikiaye hayo MANENO YANGU, na kuyafanya, atafananishwa na MTU MWENYE AKILI, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba"
Kwa hiyo neno la Mungu linapongia ndani ya mtu ni kwamba Mungu ameachilia akili ndani ya mtu, mtu anapolitenda hilo neno anaonekana kama mtu mwenye akili.
USHAHIDI WA 3
(Kumbukumbu la Torati 4:6)
"Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili"
Mungu aliwaambia wana wa Israeli kuwa neno lake ndilo hekima na akili, ili wawe taifa lenye watu wenye akili lazima wajifunze kutendea Kazi neno la Mungu.
NB: Neno la Mungu ni chanzo cha akili kadiri unavyozidi kuliweka neno la Mungu kwa wingi ndani yako ndivyo akili za aina mbalimbali zinaongezeka ndani yako, kwa maana nyingine ni kwamba ukikosa neno la Mungu kuna aina za akili unazikosa au unakuwa hauna aina fulani za akili.
Hivyo basi ninakuhimiza kusoma sana Biblia na kujifunza neno la Mungu kutoka kwenye vyanzo tofautitofauti kama vile mahubiri ya watumishi wa Mungu, vitabu vilivyoandikwa na watumishi wa Mungu nakadhalika.
0 Maoni